Kamanda Mpya wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Lazaro
Benedict Mambosasa amewapa salamu watu wote wanaojihusisha na vitendo
vya kihalifu Jijini humo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza na Waandishi wa habari katika makao makuu
ya kanda ya jeshi hilo, Kamanda Mambosasa ametamka kuwa yeye yupo
kikazi zaidi na hivyo wahalifu watafute mikoa mingine ya kukimbilia na
sio Dar es salaam.
Hata hivyo Mambosasa ameeleza kuwa katika kipindi chake atahakikisha
Polisi wake wanafanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kuepuka uonevu kwa
Wananchi.
Aidha Mambosasa amemaliza kwa kusema kuwa yote hayo yatafanikiwa endapo
wananchi watashirikiana na Jeshi la Polisi ili kupafanya Dar es salaam
kuwa sehemu ya amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment