Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa
washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa
ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi,Rukwa na Kigoma
akisisitiza jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.
Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais
TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akizungumzia umuhimu wa mfumo huo katika
kuleta mageuzi ya kiutendaji kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa
kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka
mikoa ya Katavi,Rukwa na Kigoma.
Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka PS3 bw. Desderi Wengaa akizungumza wakati wa hafla ya Kufunga mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma.
( Picha na Frank mvungi-Maelezo
Frank Mvungi – Maelezo
Serikali imewataka watumishi wa
umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na kutekeleza majukumu yao
kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo yanayofanywa kwa kushirikina na
wadau wa maendeleo.
Akizungumza wakati akifunga
mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa mipango,bajeti na
kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Katavi, Rukwa
na kigoma ,Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya serika ni
kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi hasa
katika kuwahudumia wananchi.
“Mfumo huu sio wa majaribio hivyo
ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika mkoa na halmashuri na
kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi ambao hawakushiriki katika
mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji uwajibikaji wa pamoja”
alisisitiza Chote.
Akifafanua Dkt. Chote amesema kuwa
washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa lakutumia weledi na ujuzi
waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo yao ili azma ya serikali
kutoa huduma bora itime.
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka
Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago amesema kuwa vituo zaidi ya
elfu 22,000 vya kutolea huduma vitaunganishwa katika mfumo huo wa
Kitaifa hali itakayofanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika
kwa kuwa na mifumo bora yakutolea huduma.
“Nashukuru PS3 kwa ushirikiano
uliopo kati yake na TAMISEMI na umewezesha kutekelezwa kwa miradi yenye
tija hasa kwa wananch”.Alisisitiza Rwamiago
Akifafanua Rwamigo amesema kuwa
watumishi katika Mikoa na Halmashuri lazima waoneshe kwa vitendo namna
tofauti ya kutekelza majukumu yao kwa kutumia mfumo huo wa kielektroniki
ulioboreshwa ambao ni (web based).
Mradi wa PS3 unalenga kushirikiana
na Serikali katika kuboresha matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwemo
fedha, rasilimali watu na mifumo katika ngazi ya kutolea huduma kama
vile vituo vya Afya,Zahanati,Hosipitali na katika sekta ya elimu.
Kutokana na maboresho na
kurahisishwa kwa Teknolojia,mfumo huu mpya wa PlanRep umefanywa kuwa
‘web based’ hivyo utawezesha Halmashuri kuingiza taarifa za Mipango na
Bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa kwenye mfumo
mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI na hatimaye kuingizwa kwenye bajeti
kuu ya mwaka husika.
No comments:
Post a Comment