Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watendaji wa Mfuko
wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) pamoja na Wadau wa kampuni za simu
zilizokubali kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano
vijijini hapa nchini( hawapo pichani), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga akitoa maelezo kuhusu
huduma za mawasilino nchini kwa Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (Kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya simu Vodacom Bw. Ian Ferrao(Kushoto), wakisaini
mkataba wa ujenzi wa miradi ya mawasiliano ya simu katika Sehemu za
mipakani na maeneo maalumu.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (Kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya simu Halotel Bw. Le Van Dai (Kushoto), wakisaini
mkataba wa ujenzi wa miradi ya mawasiliano ya simu katika Sehemu za
mipakani na maeneo maalumu.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (Kulia) na Eng. Cecil
Nkomola kutoka kampuni ya simu Tanzania (TTCL) Kulia, wakisaini
mkataba wa ujenzi wa miradi ya mawasiliano ya simu katika Sehemu za
mipakani na maeneo maalumu.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (Kulia) na Mkurugenzi wa
Mawasilino wa kampuni ya simu Airtel Bi. Beatrice Singano (Kushoto),
wakisaini mkataba wa ujenzi wa miradi ya mawasiliano ya simu katika
Sehemu za mipakani na maeneo maalumu.
Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akiwa katika picha ya
pamoja na Watendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote pamoja na Watendaji
wa kampuni zinazotoa huduma za simu nchini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Watendaji wa Mfuko wa
Mawasiliano kabla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa miradi ya mawasiliano
ya simu katika Sehemu za mipakani na maeneo maalumu.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (WUUM)
Serikali kupitia Mfuko wa
Mawasiliano kwa wote (UCSAF) imesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa
miundombinu ya mawasiliano ya simu katika Sehemu za mipakani na maeneo
maalumu ili kuweza kufikisha huduma bora za Mawasiliano.
Akizungumza katika hafla hiyo
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema
kupitia utiaji saini wa kampuni tano za mawasiliano ya simu nchini
kutawezesha kata 75 za vijijini kufikiwa na huduma za mawasilino ya
simu.
“Lengo ni kuendelea kutoa huduma
bora za mawasiliano kwa wananchi, leo tumesaini mkataba huu
utakaogharimu kiasi cha pesa sh. Bilioni 10.4 ili kujenga miundombinu
bora na kukamilika kwake kutawanufaisha takribani wananchi Milioni 3.4,”
amesema Profesa Mbarawa.
Aidha, Profesa Mbarawa
amezipongeza kampuni tano za mawasiliano ya simu zilizokubali
kushirikiana na Serikali katika kufikisha huduma za mawasiliano katika
maeneo ambayo yanaonekana hayana mvuto wa kibiashara hapa nchini.
“Nazipongeza kampuni za Simu kwa
kuwa na muitikio wa kuungana nasi katika kuboresha huduma hizi,
mmeonyesha moyo wa upendo kwa watanzania wenzetu ambao na wao wanahitaji
huduma za uhakika za mawasiliano,” amesisitiza Waziri Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa pia ameahidi
kutoa ushirikiano kwa kampuni hizo endapo zitakutana na changamoto
wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ili ikamilike kulingana na
makubaliano ya mkataba.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga amezihimiza
kampuni za simu nchini kujenga miundombinu ya utoaji wa huduma za data
kwa 3G na 4G katika sehemu za vijijini ili kuwezesha wakazi wa maeneo
hayo kuendana na sayansi na teknolojia.
“Wakati wa utekelezaji wa mkataba
huu tuhakikishe kuwa utoaji wa huduma kwa njia ya data unaimairishwa
katika sehemu hizo ili kuwezesha watanzania wote wanapata huduma sawa na
wakazi wa mijini,” amesema Eng. Ulanga.
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(Mfuko) ulianzishwa na Serikali kwa sheria namba 11 ya mwaka 2006 ambayo
ilipewa jukumu kuu la kupeleka mawasiliano vijijini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment