Monday, 7 August 2017

Mkuu wa Samsung kufungwa miaka 12?

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini wanataka naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung Lee Jae-yong kupewa kifungo cha miaka 12 jela.
Bwana Lee anakabiliwa na mashtaka kufuatia wajibu wake katika sakata ya ufisadi, iliyosababisha rais wa zamani Park Gue-hye aondolewe madarakani.
Inaripotiwa kuwa alitoa pesa nyingi ili apate uungwaji mkono wa serikali.
Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari kufuatia sakata hiyo lakini anakana kufanya lolote baya.
Wakati wa siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi yake, waendesha mashtaka walimtaja kuwa mtu aliyenufaika kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa sakati hiyo.
Waendesha mashtaka wanamlaumu bwana Lee na wakurugenzi wengine wanne, kwa kumhonga mshirika wa karibu wa Rais Park, Bi Choi Soon-sil mamilioni ya dola ili wapate kupendelewa na rais.
Waendesha mashtaka walidai kuwa ufisadi huo ulikuwa na lengo la kupata uungwaji mkono wa serikali kwa mabadiliko ndani ya kampuni ya Samsung.

Hukumu inatarajiwa kutolewa tarehe 27 mwezi huu wakati kuzuizi cha bwana Lee kitafikia mwisho.

No comments:

Post a Comment