Watu hamsini wauawa Afghanstan
Maofisa wa serikali nchini Afghanstan wamearifu kuwa watu hamsini,
wakiwemo wanawake na watoto wameuawa na askari upande wa Jimbo la
kaskazini mwa mji wa Sar-e-Pul. Naye msemaji wa gavana wa jimbo hilo
ameiambia BCC kwamba Wapiganaji walikishambulia kituo cha ukaguzi wa
usalama katika eneo la Mirzawalang na kuingia kijijini, kisha
kushambulia kituo cha polisi cha eneo hilo ambapo wanawake na watoto ni
miongoni mwa waathirika.
Msemaji huyo aliendelea kueleza kuwa anaamini kuwa washambuliaji hao
wahusika wakuu ni muungano wa makundi ya wapiganaji wa Taliban na
wanamgambo wa kunid la Islamic State ingawa wapiganaji wa kundi la
Taliban wamekana madai hayo ikiwemo mauaji ya raia.
Taarifa zaidi zinadai kuwa wajumbe ishirini na nane wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali waliuawa
No comments:
Post a Comment