Monday, 31 July 2017
Waziri Mkuu Majaliwa amezungumza na Watumishi wa Umma wa Manispaa ya Mbeya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa
Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa
jijini Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
Baadhi ya Watumishi wa Umma,
Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin
Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo
taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji
katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa
kina na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa
wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa. (PIcha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Ummy Mwalimu:Tunaendelea kuchukua hatua kuhakikisha watanzania wanapata huduma za matibabu bila vikwazo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akikabidhi kadi kwa mmoja wa watoto waliojiunga na bima ya afya ya
watoto (TotoAfyaCard) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam leo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Taifa ya
Afya (NHIF) Spika Mstaafu Mama Anne Makinda na kushoto ni Benarld Konga
Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa (NHIF).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe wakati alipozindua bima ya watoto (TotoAfyaCard) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amezindua (TotoAfyaKadi) Bima ya Afya kwa watoto. katika uzinduzi uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam aki, Kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), kati ya Watanzania 52m waliopo sasa (2017) watoto ni 26.7m (sawa na 51%). Mtoto ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Waziri Mkuu Majaliwa:Waharibifu vyanzo vya maji kukiona cha moto
Waziri Mkuu amesema wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
"Hatuwezi kuruhusu Taifa likaangamia kwa ajili ya watu wachache wanaoharibu mazingira kwa kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji. Ni marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji, atakayekutwa atachukuliwa hatua za kisheria", amesema Majaliwa.
Mbali na hayo Mh. Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya iliyotengewa sh. bilioni 2.72 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji.
Amesema mkakati huo unatekelezwa kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Al Shabaab waua wanajeshi 24
Mapigano yalizuka baada ya wanamgambo wa Al-Shabaab kuvamia vikosi vya AMISOM mapema Jumapili katika Wilaya ya Bulamareer ya Mkoa wa Lower Shabelle kilomita 140 Kusini Magharibi mwa mji wa Mogadishu.
"Tumechukua miili 23 ya askari waliouawa wa AMISOM na askari mmoja wa Somalia kutoka kwenye eneo ambalo Al Shabaab waliweka mtego wa kuvizia na kuvamia,” alisema Ali Nur, naibu gavana wa Lower Shabelle.
Bi Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga
(katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi
katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa
Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal
Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria
hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze
kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti ,
mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati)
akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi
wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo
hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Washiriki wa mafunzo ya udhibiti
wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii
vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu
Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi
wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Watendaji kutoka Wizara ya Afya,
Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na
Rasilimali watu Bibi Deodata Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na
Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi
Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani)
katika ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika
Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za
miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017
Mkurugenzi Utawala na Rasilimali
Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu ya
masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa
ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji
wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti,
mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto)
akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye
ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo
ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo
vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za
miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua
Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria
Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao yanayofanyika katika
Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati
waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini
wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi
yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo
31.7.2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
…
Na Erasto Ching’oro WAMJW
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi.
Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii,
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika
kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema hayo wakati akifungua
mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi
vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu ya
matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka
hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni
watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa
mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika
kutimiza majukumu yao.
“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo
hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo
mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha
katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba
Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa
kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo
na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.
Vladimir Putin kukosesha ajira 755 wa ubalozi wa Marekani
Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo
Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.
Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.
Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa
Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.
Vigogo wa TFF warudishwa Rumande tena
Malinzi anayetuhumiwa na mashtaka 28 tofauti pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa na Mtunza Fedha, Nsiande Mwanga wanaokabiliwa na mashtaka matatu, wamepandishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu, Julai 31, asubuhi, chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbroad Mashauri, lakini kesi hiyo haikuweza kusikilizwa.
Mawakili wa upande wa Jamhuri ambao ndiyo walalamikaji, waliiambia Mahakama kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa hao kurejeshwa rumande hadi Julai 11.
Sunday, 30 July 2017
Polisi yafanikiwa kutibua njama ya magaidi kuangusha ndege Australia
Majasusi wa Australia wanasema kuwa walipata habari kuwa watu hao walikuwa na njama ya kutumia mabomu ya kujitengenezea nyumbani.
Waziri Mkuu Malcolm Turnbull alisema kuwa mpango huo umevurugwa katika oparesheni kali iliyofanywa na kikosi maalumu cha kukabiliana na magaidi nchini.
Watu wanne wametiwa mbaroni kufuatia misako iliyofanywa kote katika mji wa Sydney na maafisa wa polisi waliojihami wakishirikiana na majasusi.
Mwanamke anayesema mumewe na mwanawe ni baadhi ya waliotiwa mbaroni amekanusha kuwa jamaa zake wanahusika na kundi lo lote la watu wa imani kali.
Usalama umeimarishwa katika uwanja wa ndege wa mji wa Sydney na kuenezwa katika maeneo mengine ya nchi.
Rais Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini
Maoni yake yamechapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatia kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.
Korea Kaskazini baadaye ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.
Uwanja wa Ndege Songwe wanusurika kuteketea kwa moto
Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulitokea jana mchana na kaimu meneja wa uwanja huo, Jordan Mchami alisema iliwachukua takriban nusu saa kuuzima.
Alisema moto huo ulianzia katika eneo la barabara kuu ya Tanzania - Zambia umbali wa mita 600 kutoka maeneo yalipo majengo na eneo la kurukia ndege.
“Tumefanikiwa kuuzima, hakuna madhara yoyote katika eneo letu na si sahihi kusema uwanja umeungua. Ifahamike kwamba uwanja huu una eneo kubwa ambalo ni kama vile pori tu. Moto umetokea barabara kuu ya Tanzania -Zambia umbali wa mita 600 hivi hadi tulipo sisi,” alisema baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii na maeneo ya jirani kwamba uwanja huo umewaka moto.
Alipoulizwa kuhusu cha moto huo Mchami alisema ulionekana kuanzia barabarani na walipofuatilia kwa kuwauliza kina mama wanaofanya biashara ndogondogo kando mwa barabara hiyo waliambiwa kuwa waliona lori lililokuwa limeegeshwa eneo ulikoanzia hivyo wanahisi huenda mtu au watu waliokuwa katika gari hilo walirusha kipande cha sigara na kusababisha nyasi kuwaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, simu yake ilipokewa na msaidizi wake aliyesema kamanda yupo kwenye msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Tetemeko dogo la ardhi latokea Karagwe
Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa kutokea.
Ofisa wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Gabriel Mbogani amesema ili kupata uhakika wa tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa wapo makini baada ya kupatiwa semina kutokana na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye kuwa kubwa.
Ziara ya IGP Simon Sirro mkoani Singida kujua changamoto za Askari
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa
mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa
wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na
kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na
taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo
la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto
wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi wanawake baada ya
kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili
mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na
kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Na Jeshi la Polisi Nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa
pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi
hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi zake kwa weledi
katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.
IGP Sirro, amefanya ziara hiyo
ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi
hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili
kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Katika mazungumzo yake IGP Sirro,
amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na
bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha
upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.
Daraja refu kuliko yote Duniani
Shabiki avamia kiwanjani na kumtolea maneno makali Wenger
Shabiki mmoja alifanikiwa kupenya uwanjani wakati wa mchezo huo na kusema maneno makali dhidi yake akionyesha kumpinga kwake.
Hata hivyo shabiki huyo aliondolewa uwanjani na askari baada ya kuwa ameropoka maneno hayo makali dhidi ya Wenger.
Miezi michache iliyopita, Wenger aliongeza mkataba wa miaka miwili kuifundisha Arsenal licha ya kuwa mashabiki wakionyesha wazi hawamtaki au wamemchoka.
Saturday, 29 July 2017
Method Mwanjale nahodha mpya wa Simba
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
29-7-2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika marekebisho
hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe
Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua
nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye
kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na
msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye mabadiliko
hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi
kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed
Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu
hiyo.
Klabu inamshukuru
sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake
mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa
Nahodha wa Timu.
Kwa sasa kikosi chetu
kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden
Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
RC Makonda akabidhiwa ripoti ya wezi na Magari na vifaa Dar, 73 mbaroni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya ikiwa ni miezi kadhaa toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo.
Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya alisema katika opesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pump, starter na seat cover.
“Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73 tunawashikilia, Kinondani wamekamatwa watuhumiwa 29, Ilala wamekamatwa wahutumiwa 33 na mkoa wa kipolisi Temeke wamekamatwa wahumiwa 11,”
Alisema jumla ya power windows zilizokamatwa ni 40, Raidio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya magari 109, wiper switch 7, Tampa 4, left pump3, Air cleaner 1, Booster 3, show grill 6, machine za kupandisha vino 1 na tyre used 2.
Pia alisema katika mahojiano na wahutumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni namna gani na wapi wamevipata.
Wahutumiwa wote bado wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahamani kwa hatua zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)