Friday, 30 June 2017
Waziri Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda kuchunguza Mapacha mawili
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakijadili kwa umakini
na katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakiongea na
waandishi wa habari(Hawapo kwenye picha) juu ya taarifa ya kuibiwa kwa
mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es
salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
BaKari Kambi akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (Hawapo
kwenye picha) wakatati wa uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa
kwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliofanyika mapema leo katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Waandishi wa habari wa vituo
tofauti wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za
kuibiwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliowasilishwa leo na mwenyekiti wa
kamati Dkt. Charles Majige ambae pia ni Daktari bingwa wa Magonjwa
yakina mama , uliofanyika leo mapema katika ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari juu ya tuhuma za
kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi.Hasma Juma katika Hospitali ya Temeke
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa familia ya Bi Hasma
Juma Jordan Jaddah akifuatilia kwa umakini Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akisisitiza juu
ya taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi Dkt.
Charles Majige juu ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma.
NA WAMJW DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa
tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Bi. Asma Juma kuhusu
kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya
Temeke Dar es salaam.
Akipokea taarifa kutoka kwa
Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt.
Charles Majige Waziri Ummy amesema kuwa Bi. Asma Juma(29) hakuwa na
watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo
cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume
huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma
hakuwa na watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa
tumboni uliofanywa katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo”
alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
wanafamilia ya Bi. Asma wanatakiwa kumfariji ndugu yao na sio
kumkumbushia jambo hili mara kwa mara kwani litamharibu kisaikolojia na
kushindwa kutekeleza wajiu wake kwa mtoto kama mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa
sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali
walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Profesa Makame amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA
Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM
International, Bw. Rey Blumrick akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wa hatua iliyofikiwa
kwenye ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa
jengo hilo leo mchana.
Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM
International, Bw. Rey Blumrick akifafanua Jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), wakati
Waziri huyo alipokagua ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika
pichaa ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), na watendaji mbalimbali mara baaada ya kukagua ujenzi wa
Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, leo mchana.
Muonekano wa sehemu ya Jengo la 3
la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kukamilika kwake kutawezesha jengo hilo kuhudumia abiria wapatao milioni
8 na nusu kwa mwaka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la
Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na
kuelezea kuridhishwa kwake kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua
ujenzi huo Waziri Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi BAM
International anayejenga jengo hilo kuwa Serikali italipa madai yake kwa
wakati kwa kadri atakavyoyawasilisha.
“Nia yetu ujenzi huu ukamilike
ifikapo Septemba mwakani, hivyo tunamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya
ujenzi na wasimamizi kumsimamia kikamilifu ili vifaa vinavyofungwa
katika jengo hilo viwe na ubora uliokusudiwa na vidumu kwa muda mrefu”,
amesisitiza Profesa Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema kukamilika
kwa jengo la tatu la abiria la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
kutawezesha uwanja huo kuweza kuhudumia abiria wapatao milioni 8 na
nusu kwa mwaka na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii na
wageni wengi zaidi kufika nchini.
Jeshi la Laua Majambazi wanne Kibiti usiku wa kuamkia leo
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku
kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.
taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.
"Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.
Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. "
Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu hao.
Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.
Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.
Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga
wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bungeni leo Ijumaa Juni 30 2017
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha hamsini na
saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais(TAMISEMI) Mhe,Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge
katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani
Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao
cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge
katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11
leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano
wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe.Eng,Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya
wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge
la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika
kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini
Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato
Chumi akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akiteta jambo na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent
Bashungwa katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge
la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Shally
Raymond akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mbeya Mhe.Dk Mary
Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Bububu Mhe.Mwantakaje
Juma akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Washindi wa Medali za Dhahabu
katika Mashindano ya Kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika
nchini Marekani Kutoka kushoto Ndg.Rashid Kikwete,Kassi Juma Nkamia na
Abdallah Rubeya wakiwa bungeni kujifunza shughuli balimbali za Bunge.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimsikiliza Mbunge wa Vunjo Mhe.Eng.James
Mbatia katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la
11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA
Kinyerezi II Kuzalisha Megawati 30 za umeme
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani ameagiza Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha mradi wa umeme wa Kinyerezi II
unazalisha megawati 30 za umeme nchini ifikapo Desemba mwaka huu.
Kalemani amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi huo leo asubuhi (Juni 30) ili kujua hali ya utendaji.
Amesema taarifa aliyopewa tangu alipowasili ni kuwa mradi huo utazalisha
megawati 240 utakapokamilika mwakani ila 30 zikamilike Desemba mwaka
huu.
"Mradi wa Kinyerezi II tunategemea utupatie megawati 240, lakini lazima
tuanze kupata hizo mapema, kwa taarifa niliyosikia tutaanza na megawati
30 sasa niseme megawati hizo tupate ifikikapo Desemba," amesema
Kalemani.
Amesisitiza kuwa zitakazobakia apewe ratiba za utekelezaji wake ili hadi kufikia Septemba 2017 megawati zote ziwe tayari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanesco, Tito Mwinuka ameomba ushirikiano
baina ya Serikali na Shirika hilo ili kufika malengo ya agizo la Naibu
Waziri.
"Tushirikiane pamoja Tanesco na Serikali kuhakikisha fedha zinapatikana
kwa wakati ili kwamba mradi ukamilike kwa wakati," amesema Mwinuka.
Kalemani ameongeza kuwa hakutakuwa na uongezaji wa muda katika miradi
yote miwili ya Kinyerezi I na II hivyo kuwataka wahusika kufanya kazi
kwa nguvu na weledi ili kumaliza kazi.
Amesema mradi wa Kinyerezi I umefikia asilimia 35 hali ambayo
hairidhishi huku ukitegemewa kutoa megawati 185 kufikia Agosti 2017.
Ufaransa: Polisi yamkamata mtu aliyejaribu kuvamia msikiti
Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa.
Mtu huyo hakuweza kutimiza azama yake baada ya kushindwa kuvipita vizuizi vilivyokuwepo mbele ya msikiti huo.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia.
Lengo la shambulizi hilo bado halijajulikana.
Ujerumani yatinga fainali kombe la mabara, yaipiga Mexico 4 - 1
Mastaa waliohudhuria kwenye harusi ya Messi, Argentina
Sergio Busquets, Jordi Alba, Carles Puyol, Cesc Fabregas, Xavi na Samuel Eto'o wote wameonekan katika picha iliyopostiwa kwenye ukurasa wa Instagram na mke wa Puyol, Vanessa Lorenzo.
Messi amewakaribisha wenzake wote katika kikosi cha Barcelona kwenye sherehe hiyo mjini Rosario, ambako wageni wamekodiwa hoteli ya nyota tano.
Mke wa Sergio Aguero, Karina ataimba wimbo wa kwanza katika sherehe hiyo.
Messi pia ameagiza kipikwe chakula cha kiasili cha 'locro' na 'empanada' ambacho ni nyama rosti kabisa ya Kiargentina pamoja na 'maanjumati' mengine.
Messi na mpenzi wake wa tangu utotoni hatimaye wataoana baada ya kukutana tangu wana umri wa miaka mitano mjini Rosario, Argentina walipokulia na wakaendelea kuwa pamoja hata mwanasoka huyo baada ya kuhamia Hispania alipofikisha umri wa miaka 13 kwenda kujiendeleza kisokaa. Na sasa wamerejea nyumbani kwao kabisa kwa sherehe hiyo kubwa kesho.
Messi na Roccuzzo, ambao wana watoto wawili, Thiago na Mateo, watafunga ndoa yao katikati ya mji wa Rosario, Santa Fe.
Thursday, 29 June 2017
Mawakili wapya wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa
sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema
hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya
wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika
viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada
ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar
es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa -Maelezo
Na. Eliphace Marwa – Maelezo
29/06/2017
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.
Ibrahim Hamis Juma amewataka Mawakili wapya kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili ya taaluma ya uwakili na kutumia taaluma zao kwa kutoa msaada wa
kisheria kwa jamii.
Aliyasema hayo leo Jijini Dar es
Salaam wakati wa Sherehe za 56 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya
248 iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu amewahimiza
Mawakili wapya kujiendeleza kitaaluma kwa sababu kuwa wakili sio mwisho
wa taaluma kwani wanahitajika kusoma sheria za nchi mbalimbali Duniani
ili kuweza kuingia mikataba ya kimataifa.
Alisema mawakili wapya wanatakiwa
washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani
wakienda kinyume haki itapotea.
“Mawakili wote wanatakiwa kuwa
waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika
kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali wawe mawakala wa kutenda
haki,” alisema Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu aliwataka
mawakili hao kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa
haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya mawakili katika maeneo ya nje
ya miji.
Naye Rais wa Chama cha Wanasheria
cha Tanganyika (TLS) Tundu Lissu amewataka Mawakili hao kutumia taaluma
hiyo katika kuisaidia jamii kujua haki zao na utawala wa sheria japo
kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya sheria nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)