Uchaguzi wa viongozi wa Chama
cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni uliokuwa
ufanyike Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa umesogezwa mbele hadi
Juni 4.
Uamuzi wa kusogeza mbele
uchaguzi huo umetokana na mwitikio mdogo wa uchukuaji fomu kwa wagombea.
Muda wa uchukuaji fomu sasa umeongezwa hadi Mei 7 mwaka huu.
Fomu kwa ajili ya wagombea
zinatolewa kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni
(KIFA) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Ada ya fomu kwa wagombea wa
nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini
Msaidizi na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000.
Ajenda ya uchaguzi itatanguliwa
na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji, Kamati ya
Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na
matumizi.
Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan Mambosasa.
Kamati ya Utendaji ya TAFCA Kinondoni inayomaliza muda wake inaongozwa na Mwenyekiti Eliutery Mholery (0715 621 667) na Katibu Mkuu wake Mbwana Makata (0655 520 129).
IMETOLEWA NA TAFCA KINONDONI
No comments:
Post a Comment