Siku kadhaa baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani kutangaza zawadi ya
Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa
watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji
yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji, Basi hii Leo
Mei 31, 2017 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro ameongeza dau hilo
mpaka kufikia shilingi Milioni 10.
Katika mkutano wake wa Kwanza na Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam
tangu aapishwe, IGP Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo
linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao.
Kwamujibu wa ripoti Polisi imepata picha za baadhi ya watuhumiwa na fununu za mahali wanapopenda kutembelea mara kwa mara.
Kamanda Lyanga aliwataja watuhumiwa hao pamoja na mwanzilishi wa mtandao
huo wa mauaji kuwa ni Abdurshakur Ngande Makeo, Faraj Ismail Nangalava,
Anaf Rashid Kapera, Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa.Wengine ni Shaban Kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Salim Mtulula, Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame.
Hata hivyo ripoti za jeshi hilo zinasema, waimegundua kuwa watuhumiwa hao hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa cha Saninga katka kijiji cha Nchinga na kijiji cha Mfesini kata ya Nyamisati pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
IGP Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwafichua watuhumiwa wote wa mtandao ambao unahatarisha hali ya usalama Mkoani humo na nchi nzima kwa UjumlaType a message
No comments:
Post a Comment