Mtaalam
wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. David Plotner
(kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa
TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee (katikati) na
Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo
yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya
Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Afisa
TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee akitoa mafunzo
ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya Utafiti
wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya
utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa
Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi
Agosti, 2017.
Mratibu wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bi. Hellen
Hillary (kushoto) kwa upande wa Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa
utafiti huo kwa upande wa Tanzania Zanziar Bi. Nuru Masoud (kulia)
wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima
unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Meneja
wa Takwimu za Jamii Bi. Sylvia Meku (katikati) akiwaelekeza washiriki
wa mafunzo ya awali ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima
Bw. Frank Mapendo (kushoto) na Jocelyne Rwehumbiza (kulia) wakati wa
mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar
es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia
kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Mwananchi
kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam akijibu maswali kutoka
kwa Mtakwimu Bw. Stephen G. Cosmas wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati
wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya
Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
Mtakwimu
Bi. Hellen Mtove wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimhoji mwananchi kutoka
kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati wa majaribio ya Dodoso
litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima
unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.(PICHA ZOTE NA VERONICA
KAZIMOTO)
No comments:
Post a Comment