Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo katika
maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya
St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali
nchini wakirudia kiapo cha uuguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi
iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani
Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi akiwakaribisha wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini
pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya
wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi,
Mkoani Singida.
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali
nchini wakiandamana na kuonyesha ujumbe mbalimbali mbele ya Mgeni rasmi
Waziri wa Afya Ummy Mwakimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi
iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani
Singida.
Waziri wa Afya Ummy Mwakimu
akisaini zawadi ya mafuta ya alizeti aliyopewa na wenyeji wake
halmashauri ya Itigi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika
kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuajiri watumishi
wa idara ya afya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi ambao
wameondolewa katika utumishi wa umma kwa kukosa sifa ya kuwa na vyeti
halisi baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati
wa maadhimsho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa imefanyika
katika hospitali ya St. Gasper, Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri Ummy amesema serikali
inatambua mzigo mkubwa wa majukumu kutokana na uhaba wa wauguzi ambao
umesababishwa na baadhi yao kuondolewa katika utumishi kwa kukosa vyeti
halisi na hivyo imetenga bajeti ya kuajiri wauguzi wa kutosha nchini
huku akiahidi kutoa kipaumbele kwa mkoa wa Singida.
“Kuna baadhi ya Zahanati na vituo
vya afya vimefungwa kwa kutokana na sakata la vyeti feki, lakini pia
tunatambua kuwa wauguzi hamtoshi na hivyo kupelekea muuguzi mmoja kutoa
huduma kwa wagonjwa wengi, hali hii inapunguza ufanisi wenu na kuwanyima
haki ya kupumzika”, ameongeza Waziri Ummy.
Aidha ameagiza waajiri wa
utumishi wa umma na hasa halmashauri zote nchini kupeleka maombi ya
watumishi wa kada za afya ili wizara iweze kutangaza nafasi hizo zijazwe
na watanzania wenye sifa huku akisisitiza kuwa nia ya serikali ya awamu
ya tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
“Serikali imegawa vitanda 25 vya
wagonjwa, magoro 25 na mashuka kwa kila halmashauri nchini huku bajeti
ya wizara ya afya ikipanda kutoa trilioni 1.9 mwaka jana hadi trilioni
2.2 kwa mwaka wa fedha 2017/18, bajeti hii itasaidia kupambana na
changamoto za sekta ya afya nchini nah ii ni ishara kuwa serikali
imedhamiria kuimarisha afya za watanzania” amefafanua Waziri Ummy.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha
Wauguzi Tanzania Pulo Magesa amewataka wauguzi kuto muangusha waziri
wao wa Afya kwa kuwa amekua mstari wa mbele kuhakikisha wauguzi na
watumishi wote wa Sekta ya Afya Nchini wanafanya kazi katika mazingira
yanayoridhisha.
Magesa amesema serikali inaweka
mazingira mazuri kwa kutenga bajeti ya kutosha ila ufanisi wake
utaonekana endapo watumsihi wa sekta ya afya hasa wauguzi ambao ndio
muhimili wa vituo vya huduma za afya mfano hospitali, zahanati na vituo
vya afya watazingatia misingi ya uadilifu, upendo na weledi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi amesema wauguzi wanaweza kupunguziwa mzigo wa kupata
wagonjwa wengi hasa kwa magonjwa yanayozuilika endapo kutaanzishwa mfumo
wa utoaji wa huduma za uuguzi kwa ngazi za kaya ambapo kila
mwanafamilia atapewa elimu ya kuzuia baadhi ya magonjwa.
Dkt. Nchimbi amesema mfumo huo wa
uuguzi kaya uendeshwe mpaka kwenye taasisi za elimu hasa shule za
msingi na sekondari ili jamii iweze kuzuia kwa kiwango magonjwa yote
yanayozuilika na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa .
Aidha amemshukuru Waziri Ummy kwa
kuunga mkono wazo hilo na kukubali kuanza kulifanyia kazi huku akiahidi
kutoa ushirikiano kwa kuwa mkoa wa Singida utatumika na sehemu ya
utafiti wa mfumo huo ili kufahamu ufanisi wake
Maadhimisho Siku ya Wauguzi
Duniani ni kukumbuka ya muasisi wa taaluma ya uuguzi Bi.Florence
Nightngale aliyezaliwa Mei 12 mwaka 1820. Wakati wa sherehe hizi huwa
mishumaa inawashwa kama ishara ya upendo na utumishi bora moyoni mwa
muuguzi. Muasisi huyu ndiye aliyefungua chuo cha kwanza cha uuguzi
nchini Uingereza.
Bi Florence alianza kutoa huduma
ya afya mwaka 1844 na mwaka mmoja baadaye kulitokea vita na yeye akawa
anahudumia majeruhi kwa kutumia mishumaa nyakati za usiku kwa vile
hapakuwepo na nishati yoyote wakati huo. Bi Florence kwa huduma yake
hiyo ya kutibu majeruhi wa vita aliweze kupunza vifo kutoa asilimia 42
hadi asilimia mbili (2).
Wauguzi waliokuwepo kwenye
maadhimisho hayo kutoka mikoa mbalimbali nchini walirudia kiapo chao cha
uuguzi ambacho sehemu mojawapo inasema “Naapa mbele ya Mungu na mbele
ya mhadhara huu, kuendesha maisha yangu na kutekeleza wajibu wangu wa
kazi kwa uaminifu. Sitafanya vitendo vyo vyote vile vilivyo viovu na
sitochukua au kutoa dawa ye yote ile ninayoifahamu kuwa ina madhara”.
Awali wauguzi, viongozi
mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini pamoja na wananchi
waliohudhuria maadhimisho hayo walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka na
kuwaombea wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa shule ya Lucy city
ya Mjini Arusha waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya ya gari
iliyotokea hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment