Rais mstaafu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
amechaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Baraza la Kimataifa la
Wakimbizi.
Rais Kikwete amechaguliwa kushika wadhfa huo wakati akiwa bado ni
Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa
Majanga ya Afya (High-Level Panel on Global Responses to Health Crises).
Itakumbukwa kuwa mwaka juzi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon alimteua Rais Kikwete kushika wadhfa huo.
Na sasa amekuwa tena kiongozi wa ngazi ya juu wa baraza hilo la
kimataifa, ambapo katika nafasi hiyo atakuwa na wenyeviti wenza ambao
ni Hina Jilani kutoka Pakistan na Rita Sussmuth kutoka Germany.
Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1951 ni Lloyd Axworthy kutoka Canada
No comments:
Post a Comment