Wednesday, 17 May 2017

Wazee Simba waunga mkono udhamini wa SportPesa

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Wazee Wanachama wa Simba SC, Felix Makua amesema Kupitia kikao chao cha Mei 15, 2017 waliadhimia kwenda kumuona Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ili wamueleze kuhusu baadhi ya viongozi wa Simba wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa Serikali ambao wanataka kutumia mamlaka yao na pesa (rushwa) kuiuza klabu hiyo ambapo suala hilo kwa sasa lipo Takukuru na viongozi hao wameshaanza kuhojiwa.
Mzee Makua amezungumzia pia suala la Katiba ya Simba kutofanyiwa marekebisho huku wakielekeza kilio chao kwa Waziri mwenye dhamana, Dkt. Harrison Mwakyembe ili aweze kulishughulikia mapema kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo.
Aidha wazee hao wamesema kuwa anayebeza udhamini wa Kampuni ya Michezo ya Bahatinasbu, SportPesa kwa Simba basi mtu huyo hafai ndani ya klabu hiyo huku wakimuomba Rais Aveva aendelee na motto huo huo wa kufanikisha dhamini mbalimbali.

Akizungumzia suala la udhamini wa mfanyabaishara Mo Dewji ndani ya Simba, Mzee Makua amemtaka aiheshimu klabu hiyo huku akikanusha madai ya Mo kuidai Simba mabilioni ya pesa.

No comments:

Post a Comment