Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa (MNH), Profesa Lawrence Museru
akizungumza na wauguzi leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani
ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.
Baadhi
ya Wauguzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Museru katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wauguzi wakirudia kiapo kwamba wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uadilifu.
Muuguzi wa Muhimbili, Furaha Tada akitoa mada kwenye maadhimisho hayo leo.
Wauguzi wakifuatilia mada iliyowasilishwa na mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo.
Philonem Kaongo ambaye ni Muuguzi Mkunga akitoa mada kwenye maadhimisho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru akipokea risala kutoka kwa Debora
Bukuku baada ya kuisoma kwenye maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Sebastian Luziga akizungumza kwenye maadhimisho hayo leo.
Uongozi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umesema utaendelea kuboresha
maslahi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo na kushughulikia tatizo la
upungufu wa wauguzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru ameyasema hayo leo
katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, Tawi la Muhimbili ambayo
huadhimishwa Mei 12 kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu “ Wauguzi Mbiu
ya Kufikia Malengo Endelevu ya Milenia.”
Profesa
Museru amesema Serikali ipo bega kwa bega na hospitali hiyo katika
kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. “Serikali imeahidi kutatua tatizo la
upungufu wa wauguzi katika siku chache zijazo,” amesema Profesa Museru.
Amesema
uongozi wa hospitali unashughulikia posho za wauguzi na pia kuboresha
mazingira ya kazi ili wauguzi watoe huduma bora kwa wagonjwa.
“Pia uongozi wa muhimbili utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ili wafanye kazi wa ufanisi,” amesema Profesa Museru.
Awali
mwakilishi wa wauguzi, Debora Bukuku alisoma risala ikielezea
changamoto mbalimbali zikiwamo mazingira magumu na hatarishi ya kazi na
pia kupitia risala hiyo waliomba wapatiwe posho za sare pamoja na
kuboreshewa maslahi mengine.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi amewataka madaktari na wauguzi kuendelea
kuandika machapisho ambayo yanaeleza mafanikio na changamoto za utoaji
huduma zilizopo katika hospitali hiyo.
“Bila
kuandika machapisho, hakuna atakayeona mafanikio yetu. Hii ni hospitali
ya Taifa ambayo inategemewa na hospitali nyingine kujifunza mambo
mbalimbali. Hivyo nawapongeza wauguzi kwa kuandaa mada mbambali na
kuziwasilisha kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani,” amesema
Profesa Museru.
Katika
kongamano hilo wauguzi na wataalamu wengine waliwasilisha mada
mbalimbali kuhusu wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa na jinsi ya
kuboresha huduma kwa wagonjwa wa kansa, figo na kutoa huduma bora kwa
wagonjwa wa magonjwa ya dharura na ajali.
Muuguzi
Mkunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Philomen Kaongo katika
kongamano hilo alizungumzia jinsi ya kuzuia na kutibu ugonjwa wa kansa.
No comments:
Post a Comment