…..
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo,
ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki
wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017
wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki
semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin
kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko kwenye hatua za awali za
mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa
bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli
kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu kujua vyanzo vyake
vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa
kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna
Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine
ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.”
Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo
nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni
pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua
semina hiyo.
Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa
habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato
Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017
na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard
Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya
ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye
ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
“Najua kihistoria linapokuja
swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala
hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali
kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo
waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha
umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Bwana Kayombo amesema, TRA kwa
niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za
serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya
na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa
kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari
watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi
ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
No comments:
Post a Comment