Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mwalimu alisema nchi yetu inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata hivyo kuna uwezekano wa ugonjwa huo kuingia hapa nchini kutokana na mwingiliano wa watu, hasa wasafiri wanaotoka na kuingia.
Alisema kutokana na hali hiyo wizara inaendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa huu usiingie hapa nchini.
"Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu, waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu. Aidha Wizara inaendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini," alisema Ummy.
Vilevile alisema wizara inaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha ufuatiliaji na kutekeleza mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo ili usiingie hapa nchini.
No comments:
Post a Comment