Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki wanatarajia kufanya mazungumzo ya pamoja baina yao katika
Mkutano wa kawaida wa 18 utakaofanyika kesho Mei 20 Ikulu jijini Dar
es salaam.
Mkutano huo unatarajiwa kupokea
ripoti ya usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Benjamini William Mkapa kuhusu mgogoro wa nchini
Burundi.
Mambo mengine yatakayozungumzwa
katika mkutano huo ni pamoja na taarifa na maelekezo mbalimbali
yaliyotolewa katika mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo.
Masuala hayo ni pamoja na namna ya
kuwezesha uundaji wa magari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na
kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya, mapitio
kuhusu sekta ya nguo na ngozi.
Aidha masuala mengine ni pamoja na kuzuia ama kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kutoka nje.
Wakuu hao wa Nchi pia wanatarajia kujadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa nchi wananchama.
Aidha, katika Mkutano huo wa
18 Tanzania itakabidhi nafasi ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo iliyoishika
kwa muda wa miaka miwili kwa nchi ya Jamhuri ya Uganda.
No comments:
Post a Comment