Kuapishwa kwa Macron kunakuja huku akiwa anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kufufua uchumi na kuleta pumzi mpya ya uhai ndani ya umoja wa Ulaya
Macron anaapishwa kuchukua nafasi ya rais anayemaliza muda wake, Fancois Hollande ambaye miaka yake mitano madarakani ilikumbwa na ukosefu mkubwa wa ajira na mashambulizi ya kigaidi.
Baada ya kupita katika zulia jekundu katika Ikulu ya Elyzee katikati mwa jiji la Paris, Macon na Hollande watakuwa na mazungumzo ya faragha katika ofisi ya rais ambako Macron atakabidhiwa namba za kufungua silaha za Nuclear za Ufaransa.
No comments:
Post a Comment