Thursday, 18 May 2017

Burundi: Vijana wanaounga mkono Serikali wauawa

Bujumbura ni baadhi ya maeneo yalioathiriwa zaidi na machafuko ya 2015
Watu watatu wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi la vijana linalounga mkono serikali ya Burundi wameuawa kufuatia mlipuko wa guruneti mjini Bujumbura, polisi wanasema.
Kamishna wa polisi wa manispaa, Bonfort Ndoreraho aliiambia AFP kuwa bado haijabainika ni nani aliyewashambulia wanachama hao wa Imbonerakure.
Mtu asiyetaka kujulikana alliambia AFP kuwa bado haijabainika ikiwa ilikuwa ni shambulio au ajali tu.
Kikundi cha Imbonerakure kinasemekana kuwa cha wanamgambo ambao wamekuwa wakiwashambulia wale wasiomuunga mkono Rais Pierre Nkurunziza na chama cha CNDD-FDD.



AFP inaripoti kuwa mlipuko huo ulifanyika jumatano katika nyumba moja katika wilaya ya Musaga ambayo ndio makao makuu ya vijana hao.
Takriban watu 439 waliuawa na wengine elfu 240 kutorokea nchi jirani baada ya machafuko kuzuka mwaka wa 2015, kufuatia uamuzi wa Nkurunziza wa kuongeza hatamu yake uongozini kwa miaka 10.

No comments:

Post a Comment