Monday, 5 December 2016

Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu

kiru1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
kiru2
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) akizindua rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
kiru3
Baadhi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa nchini wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) alipokuwa akizindua rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
kiru4
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakishangilia baada ya kukata utepe kuzindua rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
kiru5
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wapata maelezo kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi kuhusu kazi  zinazofanywa na Idara ya Uendezaji Maadili wakati wa Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment