Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo akizungumza na Wahasibu
kutoka Taasisi za umma na binafsi waliohudhuria katika hafla ya kutoa
tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma
ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akizungumza na Washindani
wa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015 kutoka Taasisi za umma
na binafsi takribani 56, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu
50, Bw. Christopher Lupama akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya
Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo baada
ya kukabidhiwa tuzo ya Taarifa nzuri ya Fedha kwa mwaka 2015 kwa upande
wa Wizara na Idara zake, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu
50 Bw. Christopher Lupama akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Bw. Pius Maneno baada ya
kukabidhiwa tuzo ya Taarifa Bora ya Fedha kwa mwaka 2015, ambayo imevuka
asilimia 75 kwa ubora, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa walioambatana na Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu
50, Bw. Christopher Lupama, wakipeana mkono na Viongozi wa Serikali na
Bodi ya NBAA baada ya kupokea tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka
2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje
kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu
50 Bw. Christopher Lupama, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na Maafisa alioambatana nao wakati wa kupokea tuzo ya Taarifa Bora ya
Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA)
kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akiwa katika picha ya
pamoja na na washindi wa tuzo ya Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015,
katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi (kulia) na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo
wakibadilishana mawazo wakati wa zoezi la kuwakabidhi washindi wa Tuzo
ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, tukio lililofanyika katika
Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la
Dar es salaam.
Wahasibu nchini wametakiwa
kuzingatia viwango vya uhasibu vinavyotakiwa na kukubalika kitaifa na
kimataifa wakati wa kuandaa taarifa za fedha kwa kuzingatia maslahi ya
Taifa.
Wito huo umetolewa na Kamishna
Msaidizi Sera, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi,
wakati akikabidhi tuzo za Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015/2016,
kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James tukio lililofanyika
katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichoko Bunju, nje kidogo
ya Jiji la Dar es salaam
Katika tukio hilo ambalo
liliambatana na kufungwa kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu unaojumuisha
nchi za Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Mipango, kupitia Fungu 50,
imepata tuzo ya kuandaa vitabu bora vya mahesabu vinavyokidhi viwango
vilivyowekwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).
Bw. Msangi amesema kuwa taarifa
za fedha hutumika katika matumizi mbalimbali katika Sekta ya umma na
binafsi, hivyo iwapo taarifa hizo zitakuwa katika viwango vyenye ubora
zitaongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Amesema kuwa taarifa hizo pia
hutegemewa na wawekezaji katika kupanga maamuzi yao ya uwekezaji hapa
nchini hatua itakayosaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya
viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Bw.
Pius Maneno, amesema kuwa, kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji
wa taarifa za fedha kwa upande wa Taasisi za Umma na Binafsi mwaka huo
ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Mwaka uliopita Taasisi nyingi za
umma zilishindwa kufikia asilimia 75 ambacho ndicho kiwango cha chini
kabisa cha Taasisi kuingia katika ushindani wa Tuzo ya taarifa bora ya
Fedha ya mwaka, lakini kwa mwaka huo, Taasisi za Serikali zilizokidhi
kiwango hicho ni zaidi ya Asilimia 50.” Aliongeza Bw. Maneno.
Aidha, amesema kuwa katika
kutafuta mshindi wa Tuzo hiyo taasisi mbalimbali zimehusishwa ikiwemo
Mamlaka ya Bima Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya
Utawala wa Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya matokeo
kuthibitishwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA
Prof. Isaya Jairo amebainisha faida za tuzo ya taarifa bora ya fedha
kuwa ni pamoja na kujenga uwazi, uwajibikaji, uadilifu na kuwa na
taarifa ya fedha yenye viwango.
Amezitaka Taasisi nyingi
kushiriki katika ushindani ili kuboresha taarifa za fedha za Mashirika
yakiwemo ya umma na binafsi, huku akitoa wito kwa Serikali kuziagiza
Taasisi zake kushiriki kikamilifu.
Miongoni mwa wizara zilizoibuka
na ushindi wa Tuzo hiyo ni Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 ambapo
iliwakilishwa na Mhasibu wake Mkuu Bw. Christopher Lupama kupokea Tuzo
hiyo, ambaye amebainisha kuwa Tuzo hiyo imewapa nguvu ya kuendelea
kufanya vizuri katika utoaji wa Taarifa ya Fedha yenye viwango.
Taasisi 56 zimeshiriki kuwania tuzo hiyo inayoandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
No comments:
Post a Comment