Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN), kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers leo na kesho.
Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk. Hassan Abbas, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi, kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, katika mkutano huo wanatasnia watapewa mafunzo juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yao wanaifanya kazi hiyo kama ajira nyingine.
Taarifa ilifafanua kuwa katika mkusanyiko huo, mbali na washiriki kupata mafunzo, pia watapata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana-blogu.
Iliongeza kuwa mkutano huo ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalamu wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja wameandaa mafunzo hayo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.
"TBN inaendelea kuishukuru serikali kupitia taasisi zake ikiwamo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake," taarifa ilisema.
Kadhalika, imezipongeza pia kampuni nyingine zikiwamo SBL na Coca Cola pamoja na PSPF na NHIF kwa kuungana nao katika kufanikisha tukio hilo la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya.
"Kimsingi, lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii," taarifa ilisema.
Iliongeza kuwa TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hiyo katika kutoa taarifa.
"Kwa dunia ya sasa, hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa na kiburudisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kijamii
No comments:
Post a Comment