Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa
maagizo ya Viongozi wa juu na kuwatumikia wananchi kwa kupunguza
changamoto zilizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, mara baada ya
Waziri wa Nchi kushoto kwake George Simbachawene kutoa hotuba yake kwa
Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wanaounda Baraza la
Wafanyakazi la Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa
maagizo ya Viongozi wa juu na kuwatumikia wananchi kwa kupunguza
changamoto zilizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, mara baada ya
Waziri wa Nchi kushoto kwake George Simbachawene kutoa hotuba yake kwa
Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini
Dodoma.
Waziri wa Nchi George
Simbachawene akitoa hotuba kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika
katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene
amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na
kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, sambamba
na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika kikao cha
baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma,
Simbachawene amesema watumishi hao wanatakiwa kuwa na utendaji unaojali
matokeo na kuepuka utendaji wa mazoea.
Amesema wanatakiwa kuzingatia
nidhamu na utendaji wa Watumishi wa Umma,na watambue maadili ni nguzo
muhimu ya kuepuka vitendo vya ubadhilifu na rushwa mahali pa kazi.
Hata hivyo, amesema kwasasa
inafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa kwenye ofisi hiyo zinazotokana na
uhamisho, upangaji wa walimu na michakato ya teuzi mbalimbali.
Waziri huyo amesema kumekuwa na
tuhuma kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na vitendo vya rushwa na
kwamba watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali
za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Sambamba na hilo, ametaka kila
Idara na kitengo kuhakikisha kuwa zinapunguza matumizi yasiyo ya lazima
ili kuelekeza rasilimali fedha katika kutekeleza majukumu ya msingi
ambayo yataleta tija kwa Taifa.
Simbachawene amewaambia
wafanyakazi hao kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi ya
wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu.
No comments:
Post a Comment