kuelekea Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Serikali imepongezwa kwa Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi chote tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wakati wa mahojiano maalum kuhusu
maadhimisho ya miaka hamsini na tano ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika
kitaifa tarehe 9 Desemba mwaka huu.
“Tumepiga hatua kubwa katika
upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu,Afya,Maji,usafirishaji na
miundo mbinu ukilinganisha na wakati tunapata Uhuru” Alisisitiza
Chongolo
Katika Sekta ya elimu Chongolo
anabainisha kuwa Serikali katika awamu zote tangu awamu ya kwanza hadi
sasa zimekuwa zikiweka kipamaumbele katika Sekta hiyo hali iliyochangia
kuongezeka kwa shule za msingi ,Sekondari na Vyuo Vikuu .
Akifafanua zaidi Chongolo
ameongeza kuwa elimu bure ni miongoni mwa dhamira ya Serikali ya Awamu
ya tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuzidi kuendeleza azma
ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kupamabana
na maudui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasikini.
Akizungumzia kuhusu miundo mbinu
ya barabara anabainisha Tanzania ya sasa ina tofauti kubwa na wakati
Taifa lilipokuwa likipata Uhuru ambapo barabara za lami na madaraja
yalikuwa machache lakini hivi sasa Mikoa yote inafikika kwa urahisi.
Anaongeza kuwa sekta ya maji pia
imeimarika ukilinganisha na wakati wa uhuru ambapo moja ya miradi
mikubwa iliyotekelezwa na Serikali ni mradi wa maji wa ziwa Victoria
hadi shinyanga na mwingine ni ule wa upanuzi wa mitambo ya Ruvu juu na
Ruvu Chini ambayo imeanza kumaliza tatizo la maji katika Jiji la Dar es
salaam.
Aidha Chongolo aliwaaasa wananchi
kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za Taifa na miundo
mbinu iliyopo kwa maslahi ya taifa kwa kuwafichua wale wote
wanaokwaamisha au kuhujumu nia njema ya Serikali katika kuwaletea
wananchi maendeleo.
Sherehe za Uhuru huadhimishwa
kila mwaka inapofika tarehe 9 mwezi Desemba ambapo mwaka huu Kitaifa
zitafanyika Jijini Dar es salaam na Kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe mwaka mmpja uliopita.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni
“Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa,Ufisadi na Kuimarisha Uchumi
wa Viwanda kwa Maendeleo yetu.”
No comments:
Post a Comment