Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi
Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza matambezi ya hiari sehemu ya
maadhimisho ya siku ya Maadili nchini yatakayofikia kileleni tarehe 10
Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam na
Matembeze hayo yamefanyika Leo jijini Dar es salaam kuanzia kwenye
viwanja vya Karimjee na kufikia ukomo viwanja vya Mnazi Mmoja.
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi
John Kijazi( mwenye koti la bluu) akishiriki katika mazoezi ya viungo
baada ya kumaliza matembezi ya hiari ambayo yamefanyika Leo jijini Dar
es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi
Balozi John Kijazi akiwahutubia washiriki wa matembezi ya hiari ( hawapo
pichani) mara baada ya kumaliza matembezi hayo Jijini Dar es salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza mbele ya mgeni rasmi Balozi
John Kijazi (hayupo Pichani) mara baada ya kumalizika kwa matembezi ya
hiari katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kushoto ni Katibu Mkuu wa Ikulu
Peter Ilomo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) ambaye ni mwenyekiti wa Kamati
Kuu ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu,Bw.Valentino Mlowola akifafanua
jambo mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Hiari yaliyomalizikia
viwanja vya Mnazi Mmoja katikati ni Katibu Mkuu Balozi Kijazi.
Kaimu Kamishna wa Maadili
Bw.Waziri Kipacha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Balozi John
Kijazi kwenye Matembezi ya Hiari baada ya kumaliza.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi ( Mwenye koti la bluu) akiwa kwenye picha ya pamoja nabaadhi ya
viongozi na watumishi kutoka Taasisi zinazosimamia
Maadili,Uwajibikaji,Utawala Bora,Haki za Binadamu na Mapambano dhidi ya
Rushwa baada ya kumalizika kwa matembezi ya Hiari ambayo ni sehemu za
Maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yanayotarajia kufikia kileleni
Desemba 10,2016 viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi
(mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na watoto ambao
waliungana na watumishi katika Matembezi hayo yaliyofanyika Leo.
Picha Zote na Ally Mataula-Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Na Alex Mathias na Joseph Ishengoma
Serikali ya awamu ya tano imesema
kuwa imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa za kila aina ili kujenga
jamii yenye maadili na inayochukia vitendo vya rushwa kwa kufuata kauli
ya Rais wa Tanzania anayekemia Rushwa nchini.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mwandisi
Balozi John Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati
akihitimisha matembezi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili,
uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa
yaliyoanza mapema Asubuhi katika viwanja vya Karimjee na kufikia mwisho
viwanja vya Mnazi Mmoja ambayo yaliweza kuzishirikisha Taasisi
mbalimbali zinahusiana na masuala ya utawala bora kwa mara ya kwanza
kukutana.
Taasisi hizo ni Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa,
mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma, na ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa
hesabu ambazo zilikuwa hazijawahi kukutana kufanya matembezi kama hayo
nyingine ni Ofsi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora,Tume ya Utumishi wa
Umma na Tume ya Haki za Binadamu.
“Ipo mifano ya sehemu ambazo
rushwa imekithiri kutokana na vitendoi vya rushwa na ufisadi. Kiongozi
mkubwa anashindwa kumsimamia mtu aliyechini yake kama sheria ya maadili
inavyomtaka kwasababu yeye mwenyewe mikono yake si misafi,” amesema na
kuongeza kuwa , “matokeo yake hata mtu awe na mali nyingi, bado
ataendelea kula rushwa bila kikomo”.
“Serikli ya awamu ya tano
imedhamiria kupambana na rushwa ya aina zote kwa lengo la kujenga jamii
yenye maadili inayochukia vitendo vya rushwa na ufisadi ili kuweza
kuondoa rundo la rushwa ambalo lilikuwa limeanza kuikumba nchini kwa
baadhi ya watumishi kujihusisha na masuala ya Rushwa.”amesema Balozi
Kijazi
Kwa mujibu wa Balozi Kijazi,
jitihada za serikali ni kuondokana na hulka ya ubinafsi na uroho na
kujenga utamaduni na tabia ya kijitolea kwani hata awamu hii ya Rais
Magufuli inapambana na janga hilo ndio maana kila Wizara imekuwa makini
kwa watumishi wake na kuwaonya kuacha mara moja kujihusisha na Rushwa
nchini
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi ametoa
wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa
kuielimisha jamii kuhusu maswala ya maadili nchini kwa kuandika ukweli
wa mambo ili kuweza kufikisha ujumbe katika jamii zetu na kuunga mkono
kauli hii ya kupiga Rushwa.
“Natoa wito kwa waandishi wa
habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa taifa letu kwa
kuielimisha jamii kuhusu kujenga, na kukuza maadili, haki za binadamu,
uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa ili kuandika
makala ambazo zinaonesha ukweli wa kuwaelimisha wananchi kwa nguvu zote
na kuweza kuwa na jamii bora ambayo haina uroho wa Madaraka,” amesema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi,
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola ameeleza kuwa
lengo la matembezi hayo ni kutuma ujumbe kwa wananchi kuhusu kujenga na
kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano
dhidi ya rushwa.
Kamishna Mlowola amesema, kuanzia
Jumatatu ijayo, taasisi zinazohusika na masuala ya utawala bora zitakuwa
na wiki ya utoaji huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupokea
kero na malalamiko ya wananchi na kisha kuyashughulikia pamoja na
kuyatatua kwa umakini kwa kufuata haki za kila binadamu ili aweze
kusaidiwa ikiwa ana kero ambayo inamuumiza katika jamiii.
“Hii ni moja ya kampeini ya
taasisi husika kuikataa rushwa, kujenga maadili na misingi ya uadilifu
na kuhamasisha jamii kujua haki zao,” amesema.
Matembezi ya Leo ni ya mwendelezo
wa Kampeni ya maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu ambayo
yalifunguliwa Novemba 10 mwaka huu na yanatarajia kufikia kilele chake
Desemba 10,2016 na pia amewataka watumishi waendelee kufanya mazoezi ili
kujiweka fiti na sio kukomea siku ya Leo tu.
No comments:
Post a Comment