Mwenyekiti
wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania Mohamed Jaffer akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam baada ya semina ya siku
moja ya madalali wa Bima na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa sekta za Bima.
Meneja
wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana
Masalla akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara
baada ya semina ya siku moja ya madalali wa Bima iliyolenga
kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) katika Bima.
George
Haule akiwalisha mada kuhusu kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa
madalali wa sekta ya Bima wakati wa semina ya siku moja ya madalali wa
Bima iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT)
katika Bima.
Baadhi
ya washiriki wa Mafunzo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwenye
sekta ya Bima wakati wa semina ya siku kwa madalali wa Bima iliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Picha na MAELEZO- Dar es salaam
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imetoa mafunzo ya siku moja kwa Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la
kuwajengea uwezo wa kuifahamu vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili
waweze kushiriki vema na kuondoa kasoro katika ulipaji wa Kodi ya
ongezeko la Thamani kutoka Sekta ya Bima.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Diana Masalla wakati wa mkutano waandishi wa habri kwenye
semina ya siku moja kwa Madalali wa Bima( Insurance Brokers) ya
kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Alisema kuwa mafunzo hayo
yamewaelimisha wanachama hao juu ya Kodi ya zuio , utoaji wa kodi ya
ongezeko la Thamani (VAT) na jinsi ya kulipa kwa njia ya mtandao(Revenue
gateway system).
Alisema kuwa TRA imekuwa ikitoa
mafunzo hayo kwa Wanachama na Mawakala wa Bima kwa sababu kabla ya
Sheria ya Mwaka 2014 walikuwa halipi Kodi na hivyo semina hiyo imesaidia
wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya ulipajji wa kodi ya ongezeko
la thamani.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama
cha Madalali wa Bima Tanzania Mohamed Jaffer aliipongeza Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa hatua yake ya kutoa elimu kwa wanachama wake
kwani imesaidia sana kuwajengea uwezo ambao utasaidia ulipaji wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani.
Aliongeza kuwa hatua hiyo
itasaidia kuondoa makosa katika masuala ya ulipajji kodi na jinsi ya
ujazaji wa malipo ya kodi kwa wanachama wao.
Jaffer alisema kuwa ni muhimu
sana wanachama wa Chama chake kuelewa vema jinsi ya kujaza na kulipa
kodi kwani asilimia 60 ya mapato ya Bima yanatokana na madalali wa Bima
kwa kuwa wao ndio wako karibu na wateja kuliko Kampuni za Bima ambazo
zinabaki na asilimia 40.
Alisema kuwa hadi hivi Chama
hicho kina wanachama wapato 150 ambao wamesambaa Nchi nzima ambao kwa
mwaka uliopita waliweza kukusanya wastani wa shilingi bilioni 370.
Kati ya fedha hizo asilimia 18
ndio ulipwa kodi ya ongezeko la thamani na kuongeza kuwa kiwango cha
makusanyo kwa mwaka huu kinatarajjiwa kuongeza na hivyo kuongeza mapato
ya kodi ya VAT.
No comments:
Post a Comment