Wednesday, 31 August 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 01 2016

 

Mbarali kwafurika watu wa kushuhudia kupatwa kwa jua

Mbarali. Maelfu ya watu kutoka  ndani na nje ya nchi  wakiwemo wasomi na wanafunzi wametua katika mji mdogo wa Rujewa wilayani hapa, kwa lengo la  kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua kuanzia saa 4.15 asubuhi hadi saa 7.59 mchana kesho Septemba Mosi.
Tukio hilo  la kihistoria  limevuta  umati wa watu na kusababisha msongamano mkubwa kwenye mji na viunga vyake.
Aidha tukio hilo limesababisha nyumba zote za wageni katika mji huo kujaa huku watu wakiendelea kumiminika na wengi wakionekana kukosa sehemu za malazi na kuamua kurudi jijini Mbeya.

Tanzania, Ethiopia, Rwanda zawekwa kundi moja CECAFA.

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limethibitisha kwa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kuwa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania itashiriki michuano ya kwanza ya Kombe la Chalenji kwa wanawake itakayofanyika kuanzia Septemba 11, 2016 hadi Septemba 20, 2016 kwa kushirikisha nchi saba wanachama wa shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa CECAFA, michuano hiyo itafanyika jijini Jinja na Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda.

Messi kukosa mechi dhidi ya Uruguay

Kambi ya Argentina imethibitisha kuwa Messi, mwenye miaka 29, anasumbuliwa na maumivu ya misuli ya pajani ambayo aliyapata Jumapili iliyopita wakati klabu yake FC Barcelona iliifunga Athletic Bilbao 1-0 kwenye La Liga huko Uhispania.
Hadi sasa haijajulikana iwapo Messi atacheza mechi zao mbili za kufuzu kombe la Dunia za Ijumaa dhidi ya Uruguay itakayochezwa huko Mendoza, Argentina na ile inayofuatia ya ugenini huko Merida dhidi ya Venezuela siku 5 baadae.

TRL yatangaza nauli mpya treni ya Pugu

Nauli ya abiria wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam, imepanda kutoka Sh 400 ya awali hadi 600.
Tozohiyo ya nauli mpya inatarajiwa kuanza rasmi Septemba mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Ng’hwani Kudema, alisema viwango hivyo vya nauli vilivyokokotolewa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vimepanda kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.

Shule nyingine yaungua moto Manyara

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Francis Massawe.


Matukio  ya kuteketea kwa moto mabweni ya wavulana katika shule za sekondari zilizoko Kanda ya Kaskazini yanazidi kushika kasi.
  moto uliteketeza bweni la Shule ya Sekondari ya Wavulana Aldersgate, iliyopo wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.
Kuteketea kwa bweni hilo ni mwendelezo wa matukio ya aina hiyo baada ya shule kadhaa kuteketea katika mikoa ya Arusha na Manyara.

Moto wateketeza nyumba mbili Magomeni Mapipa



 Wakazi wa eneo hilo
Zimamoto wakiwa eneo la tukio 
Wakazi wa eneo hilo wakiwa katika taharuki

Moto waunguza nyumba mbili mchana huu maeneo ya Magomeni Mapipa mtaa wa Jaribu karibu na Topland bar.
Moto huo ulianza katika nyumba moja na baada ya kupamba zaidi ukaamia kwenye nyumba ya pili.

Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki aondoka hospitalini

Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki

Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki, ambaye amekuwa akipokea matibabu nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki moja, ameruhusiwa kuondoka hospitalini.
Taarifa kutoka kwa familia yake Jumanne ilisema kiongozi huyo wa zamani "yupo katika hali nzuri".
Rais mstaafu wa Kenya Kibaki alazwa Afrika Kusini

TFF yamchunguza Mavugo

Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo.


Mshambuliaji  wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, hivi karibuni alionekana kama amelijaribu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti kwenye Ligi Kuu Bara.
Katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mavugo alivunja kanuni ya shirikisho hilo baada ya kuvaa jezi namba 11.
Hii ilikuwa namba tofauti na ile ambayo aliivaa kwenye mchezo dhidi ya Ndanda ambapo alivaa namba 9 ambayo ilisajiliwa kihalali kuwa ni namba yake.
Kutokana na hali hiyo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura, aliliambia Championi Jumatano kuwa, kitendo hicho cha Mavugo kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti katika mechi mbili tofauti za ligi hiyo ni kosa kubwa, hivyo wanamchunguza na anaweza kuchukuliwa hatua.

Fedha za Kessy za usajili Yanga milioni 40

Beki wa timu ya Yanga, Hassan Kessy.

  hii ni kali ya mwaka! Baada ya mzunguko mrefu hatimaye Simba wamewaonyesha Yanga kufuru baada ya kutaka timu hiyo iwalipe shilingi bilioni moja na milioni mia tatu, kwa ajili ya kumpata beki .
Kessy, alisajiliwa na Yanga kwenye usajili huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Simba kwenye usajili ambao umejaa utata mkubwa, hata hivyo, ameshaichezea timu hiyo michezo mitatu ya kimashindano, lakini bado figisu ni ya hali ya juu.
Klabu ya Simba imetinga kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwasilisha hoja ya kuitaka Yanga kuwapa fedha ndefu ambazo zipo katika kipengele cha mkataba baina ya mchezaji huyo na klabu hiyo endapo upande mmoja utauvunja.

Dk Likwilile aondolewa Wizara ya Fedha na Mipango

  Image result for dr likwelile
Rais Dk John Magufuli leo amemteua Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na ‘kumtema’ Dk Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine..
Kabla ya uteuzi huo Doto alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Rais Magufuli amekutana Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi  Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na
Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam kuajadili
fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu. Kulia kwake ni
Rais wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akimuonyesha Rais
wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano na ujumbe wake taarifa ya maendeleo ya Miundombinu
nchini,
 walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
 Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano (wa nne kulia)  akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es salaam kuajadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa
Rais wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano, wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini kwake
kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa
Rais wa  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini
kwake kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
PICHA NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (W-UUM)

Chadema yahairisha maandamano mpaka oktoba mosi

 
CHADEMA yatangaza kuhairisha 'Operesheni UKUTA' hadi Oktoba Mosi kutoa nafasi ya mazungumzo kati ya Rais na viongozi wa Dini.

Athari za chumvi katika mwili wa bindamu

 Image result for chumvi ya kula
Chumvi ni kiungo ambacho haipiti siku bila mtu kukitumia kutokana na uwezo wake wa kukifanya chakula kuwa radha nzuri katika ulimi.
Imeelezwa kuwa mbali ya kuwa umuhimu huo lakini kula chumvi vyingi kunasababisha madhara mengi kwa afya ya binadamu.
Chumvi inapandisha shinikizo la damu. Shinikizo la juu la damu (presha) ni sababu kubwa ambayo husababisha la kiharusi(stroke),kusimama kwa moyo,shambulio la moyo na magonjwa mengine mengi ya moyo kote duniani.

Kuna

Maajabu ya mbegu za maboga katika mwili wa binadamu

 
Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa:
Huimarisha moyo na mifupa
Mbegu za maboga (pumkin seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana.
Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi.

Ndege za Kivita Kutawala Anga la Dar Kesho Septemba 1

Septemba mosi mwaka huu inataraji kuingia katika histori ya Tanzania kutokana na matukio ambayo yanataraji kufanyika siku hiyo, matukio hayo ni pamoja na sherehe za miaka 52 ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), maandamano ambayo yamepangwa kufanywa ya UKUTA na tukio la kupatwa kwa jua.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokutana na Maafisa wa Jeshi la JWTZ Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema JWTZ inapotimiza miaka 52 ni fahari kubwa hivyo tunapaswa kuwapongeza kwa kudumisha amani na mshikamano.
Alisema Jeshi hilo limejipanga kurusha angani ndege zake za kivita katika anga la Dar es Salaam, Septemba 1 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya kuanzishwa kwake.

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini

 Rais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-ju

Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.
Waziri huyo wa elimu Kim Yong-jin anadaiwa kusinzia katika mkutano wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.
Baadhi ya ripoti zinasema waziri huyo, ambaye amekuwa pia akihudumu kama mmoja wa manaibu wa waziri mkuu, alitekwa na usingizi wakati wa mkutano huo jambo ambalo lilichukuliwa kama kumkosea heshima kiongozi huyo.
Maafisa wa Korea Kusini wamesema wanaamini waziri huyo aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Julai.
Serikali hiyo inasema maafisa wengine wawili walilazimishwa kwenda kuishi maeneo ya mashambani, "kupewa upya mafunzo".

Tuesday, 30 August 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOST 31 2016


 

Ramos ashtushwa kuachwa kwa Casillas timu ya taifa ya Hispania

Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema ameshitushwa kuona kipa mkongwe wa Hispania, Iker Casillas hakuitwa kwenye kikosi hicho.
Casillas, hivi karibuni ameisaidia FC Porto kusonga mbele hadj kuingia kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Shambulio la hoteli lawaua watu 5 Somalia

Hoteli ya SYL nchini Somalia
Bomu kubwa limelipuka nje ya hoteli moja katikati ya Mogadishu karibu na lango la jumba la rais nchini humo.
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa.Kundi la wapiganaji wa Alshabab limekiri kutekeleza shambulio hilo.

TRA yaanzisha utaratibu wa wanafunzi kulipa kodi vyuoni

Mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipa kodi (TRA) Richard Kayombo

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanzisha utaratibu wa kufungua klabu za wanafunzi wa kodi vyuoni ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa elimu kwa mlipakodi katika jamii.
Akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, Mkurugenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo ameeleza lengo la kuanzisha Klabu hizo ni kutaka kuwajenga wanafunzi kuwa na misingi ya ulipaji kodi.

Multichoice Tanzania yampa mkataba wa mwaka aliyeshika nafasi ya tano olimpiki

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya Rio 2016 yaliomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika nafasi ya 5 kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume.
Katika Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania imemzawadia Alphonce Simbu shilling za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika maandalizi yake ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP yanayotarajiwa kufanyika mjini London Uingereza August 2017.

Waziri Mkuu Apokea Hundi Ya Sh. Mil. 50 Kutoka NSSF

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 50 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu.
NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake iliyoitoa  Julai 17, 2016 katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu .
Katika ajali hiyo, shule ya sekondari Lindi iliathirika kwa asilimia 34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yaliungua na kusababishia hasara ya sh. milioni 682.78.

Rais Dkt John Pombe Magufuli amekutana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya

LOZ1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
LOZ2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza  balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
LOZ3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
LOZ4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akiangalia  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara akisalimiana na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo kabla ya kufanya naye  mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
LOZ5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya  mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
PICHA NA IKULU

Serikali, wadau wakutana kujadili mapendekezo ya kulinda na kukuza Haki za Binadamu Nchini

hak1
Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
hak2
Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali za Kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
hak3
Mkurugenzi Msaidizi Masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Nkasori Sarakikya akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali za Kiraia mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi hiyo Bi. Sarah Mwaipopo.

Serikali,kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya  kikao maalumu cha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi za kiraia kwa lengo la kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Period Review).
Vilevile kikao hicho kitatoa fursa ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo ya awali kama wadau, mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei 2016 , na kuainisha sababu ambazo zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu kabla ya kupitishwa rasmi kuwa  taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9 Septemba 2016.

Lowassa: kitendo cha kukamatwa na Jeshi la Polisi kimenimarisha na kumpa nguvu zaidi za kudai Demokrasia.

 
Aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CHADEMA, amesema kitendo cha kukamatwa na Jeshi la Polisi yeye na viongozi wenzie wakati wakifanya mkutano jana, kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi za kudai Demokrasia.
Katika waraka wake alioutoa kwa Waandishi Mapema leo, Lowassa amedai anafurahishwa na jinsi wanachama wa chama hicho wanavyowaunga Mkono.

Lipumba: Mimi bado ni Mwenyekiti wa CUF, sitambui kikao cha Zanzibar

 
Prof. Lipumba amesema yeye bado ni Mwenyekiti wa CUF na alishatengua maamuzi ya kujiuzulu, hakitambui kikao kilichokaa Zanzibar na kusitisha uanachama wake.

LIPUMBA: MIMI BADO NI MWENYEKITI WA CUF, SITAMBUI MAAMUZI YA KIKAO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua ACP Sida Mohammed Himid

 index
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, ACP Sida Mohammed Himid ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara maalum za SMZ.

Arsenal kumtoa Jack Wilshere kwa mkopo

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Jack Wilshere

Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika katika kikosi cha kwanza cha timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha hilo.

Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita ,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.

Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu
.

Ulinzi waimarishwa Mbarali wakisubiri kupatwa kwa jua

Mbarali. Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune amesema ulinzi na usalama umeimarishwa kwa wageni wa ndani na wale watokao nje ya nchi watakaofika mkoani humo kushuhudia kupatwa kwa jua  Septemba Mosi.

Tukio la kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika eneo la Rujewa, wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Septemba Mosi.

Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake, Mfune amesema  maandalizi yamekamilika ikiwamo utaratibu wa kushuhudia tukio hilo ambalo halijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita.

“Tukio hili ni kubwa na la kihistoria na litawapa fursa ya kuona vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana Mbaralia,” amesema

 Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(Tanapa) Paschal Shelutete amesema tukio hilo litafungua utalii wa ukanda wa kusini.

Kupatwa Kwa Jua Kutakavyokuwa Septemba mosi mwaka huu

 Muonekano wa jua litakavyokuwa wakati wa kupatwa kwa jua.

  Septemba 1, 2016 litatokea tukio kubwa la angani ambapo kutakuwa na kupatwa kwa jua ambapo linatazamiwa kufanyika katika usawa wa anga ya Tanzania.

Tukio hilo linatazamiwa kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi 7:56 adhuhuri siku hiyo.

Mashabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani kote pamoja na wanasayansi, wanafunzi pamoja na jamii ya Tanzania wataelekea Rujewa, kusini mwa Tanzania, karibu na Mbeya, kushuhudia duara la Jua linavyobadilika kuwa mithili ya pete.

 Nchini kote Tanzania, siku hiyo mamilioni ya watu watashangaa kuona Jua kali la utosini likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na mwezi katika tukio hilo la kupatwa kwa jua. Hali hiyo italiacha jua lionekane kama pete au hilali nyembamba au mithili ya mwezi mwandamo.

Watu wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilometa 100 unaokatisha kusini mwa Tanzania, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuelekea Katavi, Mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia Msumbiji, siku hiyo wataona jua kama duara jembamba mithili ya pete, kwa vile asilimia 98 ya jua katika maeneo yao litakuwa limejificha nyuma ya mwezi. Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa usalama na watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali

1
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali
DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali
 
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini
kupatiwa tiba.
Huu ni muendelezo wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani sekta ya Afya.
Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali,
wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.
Licha ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.
Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.
Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali  kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.
Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.
Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia nakuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana yaHapa Kazi Tu kwa vitendo.