Friday, 4 August 2017
Uongozi wa Yanga wawatupia lawama bodi ya ligi na wadhamini Vodacom
Uongozi wa Yanga kupitia kwa mjumbe wa kamati ya nidhamu Salum Mkemi umesikitishwa na bodi ya ligi pamoja na wadhamini Vodacom ligi kuu Tanzania Bara kutopewa mualiko katika hafla ya kukabidhi utoaji wa vifaa vya michezo kwa msimu wa 2017/18 ambao umefanyika jana, ambapo jezi za Klabu ya Yanga zilitambulishwa na Msemaji wa Simba Sc Haji Manara
Mkemi amesema bodi ya ligi ya TFF na Vodacom ambao ndio Wadhimini wawaombe radhi kwa Yanga kutowashirikishwa kwa kutopewa taarifa yoyote kuhusu hafla hiyo na badala yake wakasema Klabu ya Yanga imeshindwa kutuma Mwakilishi.
Hata hivyo Mkemi alifika mbali zaidi kwa kusema hizo jezi zilizo zinduliwa jana sio mali ya Vodacom na kwamba wamewahujumu kwa kuzindua mali isiyokuwa yake
"Vodacom hawaja tupa jezi zile jezi wametupa wadhamini wetu Sportpesa na zimetengezwa na Kampuni ya Joma hivyo Bodi ya ligi na Vodacom wametukosesha mapato makubwa ambapo tulitaka kuzitoa siku maalumu na wadhamini wetu walikuwa wamemualika nyota wa zamani Arsenal Sol campbell kuja kuzindua jezi zetu"
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment