Real Madrid
wameendeleza ubabe kwa mahasimu wao wakubwa Barcelona kwa kuwapa kipigo
cha pili, safari hii ikiwa ni mabao 2-0 na kufanikiwa kubeba ubingwa wa
Spanish Super Cup.
Madrid iliitwanga Barcelona kwa mabao 3-1 nyumbani kwao Camp Nou, Barcelona.
Bila ya mshambuliaji
wake, Cristiano Ronaldo aliyelambwa kadi nyekundu katika mechi ya
kwanza, Madrid imeshinda kwa idadi hiyo ikiwa nyumbani Santiago
Bernabeu.
Marco Asensio alikuwa
wa kwanza kuandika bao katika dakika ya nne tu ya mchezo na Karim
Benzema akapachika la pili dakika ya 39 baada ya kumuibia mpira beki
Samuel Umtiti wa Barcelona.
Madrid imechukua ubingwa ikiwa na jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa mabao 3-1 ugenini Camp Nou.
No comments:
Post a Comment