Rais Magufuli ametoa msimamo huo wakati akitoa hotuba katika hafla ya uzinduzi na kujibu maombi yaliyokuwa katika risala ya kiwanda hicho, ambacho kilitaka kisamehewe kodi kwa muda wa miaka 10 kutokana na deni kubwa ambalo kinadaiwa katika taasisi za kifedha, zilizokopwa kama mtaji wa kukianzisha.
Sababu nyingine za kutaka kiwanda hicho kusamehewe kodi ni kutokana na mchango wake katika shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia madawati na vyumba vya madarasa katika shule za jiji hilo pamoja na kusaidia huduma za maji.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake inahimiza viwanda ili iweze kupata mapato kupitia kodi, kwahiyo haiwezi kufanya uamuzi wa kusamehe kodi na kujikosesha mapato.
"Nianze kumshukuru rmwenye kiwanda kwa kutoa misaada kwa jamii, na kwa vile mifuko ya saruji 1300 aliyoitoa nilikuwa hapa nikija nitataka mnipeleke sehemu zilipotumika. Lakini uliniomba kusamehe kodi hilo ni ombi gumu. Kwa sababu wito wa serikali kuhimiza kujenga viwanda maana yake ni kwamba serikali ipate pesa tuweze kusomesha watoto bure, kuongeza madawa hospital nk. Ninachokuomba ni wewe tu ujipange ndiyo ushindani wenyewe.
Katika hatua nyingine, rais Magufuli ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa kwa hatua hiyo ya kufanya uzalishaji na kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 100
No comments:
Post a Comment