Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa
Mawasiliano wa Afrika ya Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo ambaye alimpokea mara
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pretoria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika
Kusini tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ( SADC) akimuwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika ya
Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19
na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).
Mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo.
akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza mara baada ya
kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augastine Mahiga amesema Mkutano huo
utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama;
Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya
Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.
Pia Mkutano utapokea taarifa ya
Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC;
Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa
Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda;
Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya
Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa
Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati
ya SADC na Saharawi ya Magharibi.
Dkt. Mahiga amesema katika
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC
(SADC Double Troika Summit) Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti
kwa Mwenyekiti mpya.
Double Troika inahusisha nchi
wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini,
Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa
Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni
kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na
kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
No comments:
Post a Comment