Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka
(katikati) akimsikiliza kwa makini bw. Is’haq Al.zadjali wa Shirika la
ndege la Oman katika mkutano alioitisha kujadili masuala mbalimbali na
wahusika wa mashirika hayo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
JNIA TBII leo.
Wadau mbalimbali wa mashirika ya
ndege yanayofanya kazi kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), wakiandika mambo mbalimbali yaliyokuwa yakisemwa na
Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka alipokutana nao leo
katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TBII.
Bw. Iqbal Sajan wa shirika la
ndege la Auric (aliyesisimama) akichangia hoja kwenye mkutano wa
mashirika ya ndege ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka wa
kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha huduma.
Kaimu Meneja Uendeshaji wa Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Rose Commino (wa
kwanza kushoto) akiwafafanulia masuala mbalimbali wafanyakazi wa
mashirika ya ndege zinazofanya safari zake JNIA, katika mkutano
ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi, Bw. Johannes Munanka (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment