Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria kufungua Maonyesho
Makubwa ya Sayansi na Teknolijia yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma
fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam.
Wapili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Prakabahran Anath. Masauni
baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi
hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu
kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akimsikiliza Mwanafunzi wa
mwaka wanne fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini
Dar es Salaam, Tumaini Lutufyo (kushoto) wakati alipokuwa anatoa maelezo
ya gari la kuzima moto ambalo linatumia gesi lililotengenezwa na
wanafunzi wa chuo hicho. Masauni alifungua Maonyesho ya Sayansi na
Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali za ubunifu
uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi
zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiliendesha gari linalotumia umeme wa jua
lililotengenezwa na wanafunzi wa fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam. Masauni alifungua Maonyesho
ya Sayansi na Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali
za ubunifu uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao
kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata
chuoni hapo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufungua
Maonyesho ya siku mbili ya Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Chuo
hicho kwa lengo l kuonyesha ubunifu mbalimbali wa wanafunzi hao. Masauni
baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi
hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu
kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Dk. Prakabahran Anath
alipokua anatoa historia ya chuo hicho kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri huyo kufungua Maonyesho Makubwa ya Sayansi na Teknolijia
yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma fani ya uhandisi chuoni hapo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment