Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin
Shigela akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa
Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa
hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani
Tanga
Mhariri Mtendaji wa Tanzania
Standard Newspapers Dkt. Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano
la Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa
hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani
Tanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi
wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa
hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani
Tanga
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakazi wa na
wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema kuzitumia fursa zilizopo
katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia na kuwaacha wenyeji kuwa
watazamaji.
Waziri Mwakyembe ametoa rai hiyo
leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la siku moja la Fursa za
Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za biashara zilizopo katika
mkoa na hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga unatarajiwa
kuanza.
“Tusipojipanga leo na kuzitumia
vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa hizi zitatumiwa na
wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.
Alieleza kuwa kama kuna changamoto
zozote zinazowakabili watu wa Tanga na Watanzania kwa ujumla katika
kutumia fursa zilizopo basi ni vema Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na
wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo
ili zigeuke kuwa fursa ili Watanzania wazichangamikie.
Aidha Mwakyembe amewasisitiza
Watanzania kuwekeza katika biashara ya huduma na viwanda vya uzalishaji
bidhaana bidha ambapo vitakuwa vikihudumia ujenzi wa miradi mbalimbali
hususani bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanga,
Tanzania.
Ameeleza kuwa hivi sasa kasi ya
wageni kutaka kutumia fursa za bomba la mafuta imekuwa kubwa ambapo
ameeleza kuwa kuna baadahi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani
wamekuwa wakifanya ushawishi ili wafanyakazi na wataalamu watakaokuwa
katika mradi wa bomba la mafuta wawe wanatumia huduma za hoteli za nchi
hiyo.
Akiongea awali, Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Martin Shigela alieleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Tanga
wameendelea kujipanga kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo
Tanga kwa ajili ya kukukuza kipato na uchumi wa mkoa wa Tanga.
“Tumejiandaa vya kutosha na wakati
ni sasa na hatuna sabababu za kuchelewa kutumia fursa zilizopo”,
alieleza Mkuu wa Mkoa huku akitaja baadhi ya uwekezaji unaotarajiwa
kufanywa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya cha Saruji, ujenzi wa
hoteli, kilimo, upanuzi wa uwanja wa ndege na uimarishaji wa miundombinu
ya reli na bandari.
Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji
wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Dkt. Jim Yonaz aliwataka wananchi
na wafanyabiashara wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanakuwa na haki
na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa za ukuaji wa
uchumi wa mkoa ili wawe sehemu ya fahari ya kuirudisha Tanga ya viwanda
kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Dkt. Yonaz alieleza kuwa kuwa TSN
wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashirikiana na Serikali ya mkoa
kwa kutoa elimu kupitia magazeti ya Daily News na HabariLeo kutangaza
fursa mbalimbali zilizopo mchini ili wananchi waweze kuzifahamu na
kuzifanyia kazi.
Jukwaa la Fursa za Kibiashara
linaloandaliwa TSN ni la kwanza kufanyika katika mkoa wa Tanga na la
tatu kufanyika hapa nchini ambapo la Jukwaa la kwanza lilifanyika mkani
Simiyu na lile la pili lilifanya mkoa wa Mwanza. Aidha kwa mujibu wa
waandaji, jukwaa kama hili linatarajiwa kufanyika hivi karibuni Visiwani
Zanzibar na baadae katika mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment