Vyombo vya habari nchini Kenya vitaandaa mijadala mitatu ya wagombea urais mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.
Mijadala hiyo itafanyika tarehe tofauti za mwezi Julai.
Mjadala wa kwanza utakaokuwa wa urais utafanyika mnamo tarehe 10 mwezi Julai.
Ule wa manaibu wa rais utafanyika tarehe 17 huku mjadala wa tatu wa urais ukifanyika tarehe 24 mwezi Julai.
Mijadala yote itafanyika katika chuo kikuu cha Catholic University Afrika Mashariki kuanzia mwendo wa 7.30 usiku na itapeperushwa moja kwa moja na vyombo vyote vya habari katika runinga na redio.
Tangazo hilo lilifanywa siku ya Jumanne na Wachira Waruru ambaye ni mwenyekiti wa kamati andalizi.
Hii ni mara ya pili mjadala wa urais unafanyika nchini Kenya.
Mjadala wa kwanza ulifanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa 2013.
No comments:
Post a Comment