Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameomba muungozo wa Spika wa kuhusu ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jana.
Jana Arusha ilikuwa inaagwa miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika ajali ya gari.
Lema amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.
Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.
Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye.
No comments:
Post a Comment