Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali inayozalishwa na kikundi cha
wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kikundi hicho
Philemon Kiemi.
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha wazalishaji nyuki cha Kisaki
katika manispaa ya Singida.
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward Mashimba kwa kuhitimu
mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya kumtunuku cheti cha mafunzo
hayo.
Eneo la kikundi cha wafugaji
nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya kutosha katika kijiji cha
Kisaki, Manispaa ya Singida.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji
na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha
uzalishaji nyuki Philemon Kiemi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda Mkoa wa
Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana nchini Tanzania.
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter
Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya ufugaji nyuki
kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki Manispaa
ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.
Amesema Singida imekuwa
ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi nzima ukiwa
ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo
kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.
Mheshimiwa Pinda amesema asali
ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana pia dawa huku
akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta kuzalisha
mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata
soko la ndani.
Ameongeza kuwa kuwa wananchi
watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta milioni 35 kufuga
nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku ikiwafaidisha kwa
kuvuna asali na mazao yake.
Mheshimiwa Pinda amewaasa vijana
waliohitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kuhakikisha wanaisambaza
elimu waliyoipata kwa wenzao pamoja na wao kuwa wagujai nyuki wa mfano
katika maeneo yao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singda
Elias Tarimo amesema Manispaa ya Singida ina vikundi 16 vya uufugaji
nyuki na wafugaji nyuki wengi wakiwa katika kata za Uhamaka, Mungumaji,
Mtamaa, Mwankonko na Kisaki.
Tarimo amesema wataendelea
kuhamasisha vijana na wakazi wengi kufuga nyuki kisasa na kusisitiza
ufugaji nyuki kibiashara ndio wenye tija na manufaa kwa mfugaji.
Mmoja wa wahitimu Jacob Edward
Mashimba amesema mafunzo ni mazuri na yatawasaidia katika kutunza
mazingira kutokana na jamii imekuwa ikikata miti kwa wingi.
Mashimba amesema katika jamii
anayotoka ya kihadzabe ambayo bado inategemea asali kama chakula kikuu
elimu ya ufugaji nyuki kibiashara itasaidia licha ya upungufu wa baadhi
ya vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki.
No comments:
Post a Comment