Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI limethibitisha kuwa mmoja wa
wafasiri wake alifunga ndoa na mwajiri wa Islamic State ambaye alikuwa
akimchunguza.
Shirika hilo la kijasusi lilichukua hatua katika maeneo kadhaa ili
kubaini na kuimarisha usalama baada ya kisa hicho, FBI iliambia chanzo
cha habari cha BBC.
Daniela Greene aliwadanganya waajiri wake kuhusu ziara ya 2014 kulingana
na chombo cha habari cha CNN ambacho kilifichua habari hiyo.
Danieal mwenye umri wa miaka 38 alihudumia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kurudi nchini Marekani.
Habari hiyo ya Green ilipangwa kuwa ya siri na Jaji mmoja wa Marekani
lakini ikafichuliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu baada ya rekodi
za mahakama ya jimbo kufunguliwa.
Mtu ambaye Green alifunga ndoa naye ni Denis Cuspert ambaye ni raia wa
Ujerumani aliyebadilika na kuwa mwajiri wa Islamic State.Mnamo mwezi
Februari 2015, serikali ya Marekani ilimtaja kuwa gaidi duniani. Katika
video moja ya Propaganda alionekana akishikilia kichwa cha mtu
kilichokatwa.
Green ambaye alihudumu katika afisi ya Detroit alipewa kazi ya
kumchunguza Cuspert kulingana na CNN. Miezi sita baadaye mfasiri huyo wa
lugha ya Ujerumani alielekea nchini Syria kufunga ndoa naye.
Greene aliyezaliwa nchini Czechoslovakia aliambia wakubwa wake alikuwa
anapanga ziara ya kuwatembelea wazazi wake nchini Ujerumani. Lakini
badala yake akasafiri kuelekea Uturuki ambapo alivuka mpaka wa Syria kwa
usaidizi wa wahudumu wa Islamic state, CNN ilisema.
Wakati huo Greene alikuwa bado ameolewa na mwanajeshi mmoja wa Marekani.
Muda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria mnamo mwezi Juni 2014,
aliripotiwa kufunga ndoa na Cuspert. Alikua amewacha jina lake la usanii
Deso Dogg na kujiita Abu Talha al-Almani.
Lakini Greene alikuwa na mafakira mengine kuhusu mumewe wa pili.
Kulingana na CNN alimwandikia mtu mmoja ambaye hakutajwa nchini Marekani
:”Nadhani nimefanya kitu kibaya wakati huu”.
Siku ya pili aliongezea: ”Nipo katika mazingira hatari sana na sijui nitakuwa hapa kwa muda gani,lakini haijalishi, najuta”.
Denis Cuspert
Mwezi mmoja baada ya kuwasili Syria aliitoroka nchi hiyo na kurudi
nchini Marekani. Alikiri kwa wachunguzi kwamba alimwambia Cuspert kwamba
anachunguzwa na FBI ,kulingana na ripoti hiyo ya CNN.
Haijulikani ni vipi alifanikiwa kulitoroka eneo hilo la IS .
Greene alikiri makosa hayo mnamo mwezi Disemba 2014 kwa kudanganya
kuhusu ugaidi wa kimataifa. Alihudumia kifungo cha miaka miwili jela na
aliwachiliwa mwaka uliopita. Green kwa sasa anafanya kazi kama muhudumu
anayewakaribisha wageni katika hoteli moja ambayo haikutajwa.
No comments:
Post a Comment