Benki Kuu ya Tanzania imeamua
kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za
kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12
Mei, 2016.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya
Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, taarifa
iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza.
Uamuzi huu umechukuliwa baada ya
Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina
upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya
Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.
“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi
unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, an kwamba kuendelea kwake kutoa
huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa
hiyo imeeleza.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana
katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”
Benki Kuu ya Tanzania imechukua
uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2)
(a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
imewataka wenye amana, wadai na wadaiwa wa iliyokuwa Mbinga Community
Bank kuwa wavumilivu wakati Mfilisi kwa wakati muafaka atawafahamisha
wenye amana, wadai na wadaiwa utaratibu wa malipo wa madai, ulipaji wa
madeni na taratibu nyingine zitakazohitajika kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment