Saturday, 31 December 2016
Talaka na Gardner ni moja ya mambo 4 anayoshukuru Lady Jaydee mwaka 2016
Lady Jaydee ameitaja talaka yake kutoka kwa aliyekuwa mume wake, Gardner
G Habash, ni miongoni mwa mambo 4 anayoshukuru zaidi kwa mwaka 2016.
Jide ametumia Instagram kuyataja mambo hayo huku la nne akielezea kwa
kuweka picha ya cheti cha ndoa na talaka hiyo kutoka kwa mtangazaji huyo
wa Clouds FM.
Kwenye post hiyo pia Jide amezungumzia kwa mara ya kwanza video maarufu
ya mwaka huu iliyomuonesha Captain akijigamba kumko*oza staa huyo kwa
zaidi ya miaka 10.
“Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadhaa, au emoji
zisizo eleweka. Utoto huooooooo . Mtu aki move on hana haja kufanya
utoto wote huo , uki move on hujali chochote,” ameandika Jide.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza nchini kuzingatia kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku
Na Lucas Mboje, Dar es Saam
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa
Jeshi la Magereza nchini kuzingatia kuwa utendaji wao wa kazi za kila
siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta
ufanisi unaotarajiwa.
KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa D’Salaam.
Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi hilo kudumisha
nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi ikiwemo kutekeleza
mara moja Amri mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wao wa Jeshi.KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa D’Salaam.
“Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi letu kupata ufanisi unaotarajiwa”. Alisisitiza Kaimu Jenerali Dkt. Malewa.
Wakati huo huo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2016 ambapo Jeshi la Magereza limeweza kupata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza. Pia katika mwaka 2016 Jeshi limeweza kujenga nyumba 129 kwa njia ya kujitolea ambapo nyumba 231 zipo katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji.
Aidha, Ujenzi wa nyumba 320 za
makazi ya askari katika eneo la Gereza Ukonga maandalizi ya ujenzi
yanaendelea na ujenzi wa nyumba hizo ni kufuatia ziara ya Rais Magufuli
Novemba 29 mwaka huu ambapo alipokea taarifa ya uhaba wa nyumba za
kuishi askari wa jeshi hilo na akaagiza Jeshi la Magereza lipatiwe Tsh.
bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.
Shirika la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF wameingia Makubaliano ya Mkataba wa ubia katika mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha kusakata ngozi pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengnezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi.
Shirika la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF wameingia Makubaliano ya Mkataba wa ubia katika mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha kusakata ngozi pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengnezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi.
Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga
kimepata Ithibati na hivyo kuwa na hadhi ya kuwa Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji na mapema mwakani kinatarajia kudahili wanafunzi 30 katika
fani ya Taaluma ya Urekebishaji ngazi ya cheti.
Pamoja na Mafanikio hayo, Kaimu Kamishna Jenerali Dkt. Malewa ameelezea changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maofisa na askari, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na madeni ya wabuni na watumishi wa jeshi hilo.
Pamoja na Mafanikio hayo, Kaimu Kamishna Jenerali Dkt. Malewa ameelezea changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maofisa na askari, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na madeni ya wabuni na watumishi wa jeshi hilo.
Solo Thang ajitetea kuhusu Chid Benz
SoloThang
Msanii mkongwe wa Hip Hop Bongo Solo Thang amejitetea kuhusu
uamuzi wake wa kurekodi video akiwa na Chid Benz na kusema alichokifanya
si 'kumchoresha' bali ni kumfariji na kutomnyanyapaa maana Chid
mwenyewe ndiye aliyeomba kitu hicho kifanyike
Baadhi ya wadau wa muziki wa Bongo Fleva walitoa kauli zilizoonesha
kulaumu kurekodiwa kwa Chid Benz akiwa katika hali ya kudhoofika wakidai
kuwa ni kumdhalilisha.Kamera ya eNewz ilmtafuta Solo Thang na kumuuliza nia yake ya kupost video hiyo ilikuwa ni nini? Solo alisema kuwa hakukusudia kumchoresha Chid Benz bali Chidi mwenyewe ndiye aliyetaka kurekodiwa video baada ya kukutana naye.
Alikiba ashinda tuzo Ufaransa, awabwaga Davido, Sarkodie, Yemi Alade na wengine
Mkali huyo ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii.
“Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,” waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao.
“Mshindi, Alikiba wa Tanzania aliweza kujikusanyia jamii kubwa ya mashabiki, ‘mashabiki damu wa Alikiba’ kuweza kuuchukua ushindi. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Alikiba akiwa na sahihi katika label kubwa ya Sony, kushinda tuzo ya kimataifa ya MTV Europe Music Awards kama ‘Best African Act’ na yote kwa yote kuwa na moja ya video bora za mwaka na Aje,” wameongeza.
“The main information of this “Public Prize” is to see that our small website created in France can have links with a country like Tanzania thanks to Alikiba. Just for that, we say thank you to all those fans who have mobilized: a new link between Paris and Dar-Es-Salaam has been formed,” wamesisitiza.
Kombe la Ligi ya Comoro.
Mabingwa watetezi wa
Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ina mataji mawili ya Ligi Kuu Bara na
lile la FA kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika,
lakini wapinzani wao Ngaya Club ya Comoro wikiendi iliyopita walitwaa
taji la nne.
Ikicheza dhidi ya
Ngazi Club ya Anjuani Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Hombo uliopo
Mutsamudu kisiwani Ngazija, Ngaya ilishinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa
wa Kombe la Ligi ya Comoro.
Mataji mengine ambayo
Ngaya imetwaa msimu huu ni Ligi Kuu ya Ngazija, Kombe la Ligi Ngazija
na Ligi Kuu ya Comoro. Ngaya inafundishwa na Kocha Lucien Sylla
Mchangama mwenye Leseni C ya ukocha ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Ngaya Club
inapatikana katika mji mdogo wa Mde Bambao unaopatikana mita 400 kutoka
Kusini mwa Mji Mkuu wa Comoro, Moroni. Mechi ya fainali ya Kombe la Ligi
ilichezwa kwenye Uwanja wa Hombo uliopo Mutsamudu, Kisiwani Anjuani.
Comoro ni nchi
inayoundwa na visiwa vinne ambavyo ni Ngazija, Anjuani, Moheli na
Mayotte. Kila kisiwa hucheza ligi yake kisha mabingwa hukutana kucheza
ligi ya kupata bingwa wa Comoro katika Ligi Kuu na Kombe la Ligi.
Febuari 11, mwakani
Yanga inatarajiwa kucheza na Ngaya Club nchini Comoro mechi ya awali ya
Ligi ya Mabingwa Afrika kisha kurudiana Jumamosi ya Februari 18, mwakani
jijini Dar es Salaam.
Simba kesho kuivaa Taifa Jang’ombe
Kinara wa Ligi Luu
Bara, Simba inaondoka leo saa 1:00 asubuhi kwenda Zanzibar kushiriki
Kombe la Mapinduzi ambalo limeanza jana, timu hiyo imetamba kuendeleza
wimbi lake la ushindi kama ilivyo katika Ligi Kuu Bara.
Katika ligi kuu, Simba inaongoza ikiwa na pointi 44 ikifuatiwa na Yanga yenye 40 huku Azam FC ikiwa ya tatu na pointi 30.
Simba ipo Kundi A na
timu za Taifa Jang’ombe, URA, KVZ, Jang’ombe Boys, inatarajiwa kucheza
mechi yake ya kesho Jumapili dhidi ya Taifa Jang’ombe saa 2:30 usiku
kwenye Uwanja wa Amaan, wakitanguliwa na mechi kati ya KVZ na URA saa
10:00 jioni uwanjani hapo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema: “Tunataka kuendeleza kasi yetu ya ushindi kwenye michuano hii ya Mapinduzi, hatutazubaa, tutaifunga kila timu.
“Pia tumepanga kuwatumia wachezaji ambao hatuwatumii sana kwenye ligi ili wapate nafasi ya kuboresha viwango vyao.”
Kati ya wachezaji
ambao hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ni
Laudit Mavugo, Frederick Blagnon, Hamad Juma, Peter Manyika na Novalty
Lufunga.
Mayanja alisema wamepanga kutengeneza mzunguko wa wachezaji katika michuano hiyo na watatoa kipaumbele kwa wachezaji wa benchi.
“Tulichokipanga kama
benchi la ufundi ni kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wetu wa akiba
ambao hawakutumika sana, tunataka kuona uwezo wao wa ndani ya uwanja
baada ya kukosa nafasi ya kucheza.
Bocco awapa mkono wa mwaka mpya mashabiki Azam FC
Nahodha wa Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, amewatakia mashabiki
wa timu hiyo kheri ya mwaka mpya ‘2017’ unaoanza leo saa 6.00 usiku huu
huku akiwashukuru kwa sapoti yao waliyoionyesha mwaka huu.
Bocco ametoa kauli hivi karibuni
mara baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons walioifunga bao 1-0, huku
akifanikiwa kutupia bao hilo pekee lililorudisha morali ndani kikosi
hicho baada ya kutofanya vizuri kwenye mechi mbili za ufunguzi wa
mzunguko wa pili walipocheza ugenini na African Lyon (0-0) na Majimaji
(1-1).
“Kwanza tunawashukuru mashabiki
wetu kwa uvumilivu waliouonyesha, kwa sapoti waliotupa katika kipindi
chote kigumu tulichopitia, kama wachezaji na timu kwa ujumla tunawaomba
waendelee kuwa na moyo huo huo na pia tunawatakia kheri ya mwaka mpya
(2017) na wamalize mwaka huu vizuri, tuendelee kuwa pamoja ili kuisaidia
timu yetu iweze kufanya vizuri,” alisema Bocco wakati akizungumza na
mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz
Bocco ambaye ameipatia mafanikio
makubwa Azam FC kwa mabao yake muhimu tokea timu hiyo ikiwa madaraja ya
chini hadi kupanda Ligi Kuu mwaka 2008, aliendelea kusema kuwa wamepitia
changamoto nyingi sana kwa mwaka huu unaoisha huku akidai kuwa
wamejifunza kupitia hayo na wanachoangalia kwa mwaka mpya ni kuipeleka
mbele zaidi timu hiyo ili kufikia mafanikio.
“Changamoto zilikuwepo nyingi na
ni sehemu ya maisha, sisi kama timu tunajua mpira unachangamoto zake na
tumezipokea kama binadamu na sisi wachezaji changamoto iliyokuwa katika
kazi yetu haikuwa ndogo na tunamshukuru Mungu kwa kuweza kutusaidia
tumeweza kupigana nazo na hatukuweza kukata tamaa, kikubwa tunachofanya
hivi sasa ni kuangalia mbele zaidi ili kuipatia timu mafanikio kwa mwaka
unaokuja,” alisema.
Azam FC mbali na kuwa bingwa
mtetezi wa michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA
Kagame Cup), inamaliza mwaka huu ikiwa imefanikiwa kukata tiketi ya
kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani pamoja na taji
la Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1
kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo huo uliofungua
pazia la ligi msimu huu.
Ujio wa Mapinduzi Cup
Wakati kikosi cha timu hiyo
kikielekea mchana wa leo Jumamosi visiwani Zanzibar kwenda kushiriki
michuano ya Kombe la Mapinduzi, Bocco amesema kuwa wao kama wachezaji
wanaenda kushindana na hatimaye kurejea na ubingwa wa michuano hiyo.
“Mashindano ya Mapinduzi si mageni
kwa Azam FC, michuano hiyo si mepesi ni migumu, sisi kama wachezaji
tunaenda kushindana naamini ni sehemu moja ya msimu huu ambayo tukiweza
kuchukua kombe itakuwa ni faraja kwa klabu na mashabiki wetu pamoja na
sisi wachezaji, tukitoka huko hata tukirudi kwenye ligi tutakuwa na
morali nzuri ya kuendeleza ushindi kwenye ligi, michuano ya FA na Kombe
la Shirikisho Afrika,” alimalizia Bocco.
Ngasa kuanza ligi leo, Mbeya City ikiivaa Mbao
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili kwenye viwanja tofauti.
Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wenyeji Mwadui wataikaribisha Kagera
Sugar ya Bukoba, wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wenyeji Mbeya
City watawakaribisha Mbao FC.
Mchezo kati ya Mwadui na Kagera unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua
ukikutanisha timu jirani kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa zinazoundwa na
wachezaji wanaofahamiana vizuri.Mjini Mbeya, wenyeji wanatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wao mpya, Mrisho Ngassa waliyemsajili mwezi huu katika dirisha dogo la usajili kutoka Fanja ya Oman.
Ngassa, kiungo wa zamani wa Azam, Simba na Yanga alishindwa kucheza mechi mbili za awali za Mbeya katika mzunguko wa pili kutokana na kuchelewa kwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Aidha, Mbeya City pia inatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mshambuliaji wake, Zahoro Pazi ambaye pia alikwama kucheza kutokana na kuchelewa kwa ITC yake.
Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Toto Africans wataikaribisha Stand United na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, African Lyon wataikaribisha JKT Ruvu.
Tathmini ya Uhalifu Dar kwa Mwaka Mmzima wa 2016
Aidha, hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yanayoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti.
Akitoa tathmini ya mwaka mmoja, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 204 mwaka jana hadi 127 mwaka huu.
Idadi hiyo ni pungufu ya matukio 77, sawa na asilimia 37.7 huku matukio ya kutumia nguvu yamepungua kutoka 1,181 mwaka jana hadi 874 sawa na asilimia 26.
Kamishna Sirro alifafanua kuwa matukio ya mauaji, yamepungua kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka jana, ambapo kulikuwa na jumla ya matukio 327 wakati kwa mwaka huu ni matukio 291 pungufu ya matukio 36.
Alisema matukio ya ubakaji, yameongezeka kutoka 972 mwaka jana hadi 1030 mwaka huu, sawa na asilimia sita wakati matukio ya ulawiti yameongezeka kutoka 310 mwaka jana hadi 383 mwaka huu sawa na asilimia 23.5.
‘’Kwa matukio ya ubakaji yaliyoongezeka ni 58 na ulawiti matukio yaliyoongezeka ni 73. Lakini wizi wa watoto umepungua kutoka 26 mwaka jana hadi matukio 19 mwaka huu sawa na asilimia 27,’’ aliongeza.
Kwa mujibu wa Sirro, matukio ya uvunjaji yamepungua kwa asilimia 5.7 ambapo kwa mwaka jana kulikuwa na matukio 5,677 na mwaka huu matukio 5,355 sawa na upungufu wa matukio 322.
Kwa upande wa wizi wa magari, umepungua kwa asilimia 18.1 kutoka matukio 392 hadi 321 mwaka huu huku wizi wa pikipiki ukipungua kutoka pikipiki 2,644 mwaka jana hadi 2,191 ambapo matukio 453 yamepungua sawa na asilimia 17.1.
Wizi wa mifugo umepungua kutoka 197 mwaka jana hadi 163 mwaka huu sawa na asilimia 17.3 ikiwa ni pungufu ya matukio 34.
UFC 207: Amanda Nunes amchakaza Ronda Rousey ndani ya sekunde 48
Pambano lilianza kwa Nunes kurusha makonde mfululizo kwa Rousey yaliyomwelemea na kuchakazwa ndani ya sekunde 48 tu za pambano hilo na kumfanya mwamuzi, Herb Dean asitishe pambano.
Rousey hakuamini kama angeweza kudundwa katika muda huo mfupi na kuna wakati alitaka kuanguka wakati amesimama kutafakari kilichotokea ndani ya sekunde chache tu.
Friday, 30 December 2016
Habari Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa
Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30,
2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016.
Baadhi ya wananchi wa mji wa
Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia
mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mjini
Ruangwa Desemba 30, 2016.
Baadhi ya wananchi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye
uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano
wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya
Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
Kwa mujibu wa kifungu cha 40 (6)
cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ilipokea Rufaa moja
ya kupinga Uteuzi wa Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi
Mdogo wa Bunge Jimbo la Dimani – Zanzibar.
Rufaa hiyo ilikatwa na Mgombea wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bwana Juma Ali Juma akipinga Maamuzi ya
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani aliyemthibitisha Mgombea wa Chama
Cha Wananchi (CUF) Bwana Abdul Razak Khatib Ramadhani kuwa ni mgombea
halali.
Rufaa hiyo ilikuwa na sababu
mbili ambazo ni:- (i) Hakurudisha Fomu za Uteuzi kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na sheria na (ii) Hakudhaminiwa na Chama cha Siasa kugombea
Ubunge. Katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016, Tume
imepitia Rufaa hiyo na kuona sababu zilizotolewa na mkata Rufaa hazina
nguvu ya kisheria, kwa kuwa, Mgombea wa CUF amerudisha Fomu za Uteuzi
kwa mujibu wa sheria na taratibu. Pia, Fomu zake za Uteuzi zimesainiwa
na kugongwa muhuri wa Katibu wa Wilaya ya Magharibi B. Kwa mantiki hiyo,
Tume imekubaliana na Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani –
Zanzibar. Hivyo, Mgombea wa CUF amekidhi vigezo na uteuzi wake ni
halali na aendelee na kampeni za kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo
hilo.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha
44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume
imepokea Rufaa tatu; kutoka Kata ya Kijichi – Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, Kata ya Misugusugu – Halmashauri ya Mji
wa Kibaha, Mkoa wa Pwani na Kata ya Ihumwa – Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma, Mkoa wa Dodoma.
Kata ya Misugusugu Halmashauri ya
Mji Kibaha, Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Gasper Melkiory
Ndakidemi dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Bogasi
Hussen Ramadhani.
Katika Kata ya Kijichi, Rufaa
ilikuwa ni ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas dhidi ya
mgombea wa CHADEMA Bwana Fredrick Felician Rugaimukamu.
Kata ya Ihumwa Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Magawa Edward Juma dhidi ya maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi.
Tume katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016 imepitia Rufaa zote na imeamua ifuatavyo:
Rufaa ya mgombea wa CHADEMA Bwana
Gasper Melkiory Ndakidemi katika Kata ya Misugusugu Halmashauri ya Mji
Kibaha na ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas katika Kata ya
Kijichi, hazina mashiko ya kisheria na zimekataliwa. Hivyo, Tume
inakubaliana na Maamuzi ya Wasimamzi wa Uchaguzi wa Halmashauri hizo na
wagombea waendelee na Kampeni kwa mujibu wa Ratiba.
Kuhusu Rufaa ya Mgombea wa CHADEMA
kutoka Kata ya Ihumwa, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Tume,
imepokea barua ya Msimamizi wa Uchaguzi, Manispaa ya Dodoma, ikiwa
imeambatishwa na barua ya Mgombea wa CHADEMA kuiondoa Rufaa yake na
kwamba anakubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ambayo
yalimuengua. Pia, leo Tume imepokea barua za kujitoa Ugombea za wagombea
wa CHADEMA na ACT – WAZALENDO katika Kata ya Ihumwa. Kwa maana hiyo
Rufaa iliyokuwa imekatwa na mgombea wa CHADEMA Kata ya Ihumwa
imeondolewa kwa kuwa mkata Rufaa ameiondoa na amejitoa ugombea kabla
haijasikilizwa.
Mwisho, Tume inavisisitiza Vyama
vya Siasa, Wagombea na Wananchi wote wa maeneo yenye Uchaguzi Mdogo
kufanya Kampeni za kistaarabu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Maadili ya
Uchaguzi.
Imetolewa na:-
Jaji Mkuu (Mst. Znz) Hamid M. Hamid
MAKAMU MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
30/12/2016
Barakah The Prince ataja anachokiona kwenye label ya WCB
Alikuwa akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Wapo vizuri kwasababu wana empire yao, wana mashabiki wao wanafanya muziki wana mashabiki. Mtu yeyote ambaye yupo na empire yake na mashabiki wake ina maana anafanya kazi nzuri,” alisema muimbaji huyo.
“Kwahiyo wanajitahidi kufanya kazi nzuri na kuufikisha muziki sehemu,” aliongeza.
Hivi karibuni hitmaker huyo wa Siwezi alidai kuanzisha label yake mwenyewe iitwayo BANA na wasanii wa kwanza walio chini yake ni Lord Eyez na Naj.
Makubaliano ya kusitisha vita Syria yatekelezwa
Makubaliano ya kusitishwa mapigano kote nchini Syria yameanza kutekelezwa.
Mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi, yamesitishwa kwingi lakini kuna ripoti kuwa yanaendelea kwa kiwango kidogo katika sehemu chache tu.
Hii ni kwa sababu makundi mengine hayajashirikishwa kwenye makubaliano hayo ya amani na mapambano bado yanaendelea dhidi la makundi ya Nusra Front, YPG , na vilevile lile la IS Makubaliano hayo yaliafikiwa kwa ushirikiano wa Urusi na Uturuki yakiungwa mkono na Iran, lakini Marekani haikuhusishwa.
Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan katika kipindi cha mwezi mmoja.
Shirika la wachunguzi wa haki za kibinaadamu nchini Syria SOHR ,lenye makao yake huko Uingereza limesema kuwa maeneo mengi ya taifa hilo yalikuwa yametulia usiku kucha.
Lakini limeripoti vita vikali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Hama.
Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman ameiambia AFP: makundi madogo ya waasi
pamoja na makundi yanayotii waasi hao yanajaribu kuharibu makubaliano hayo kwa sababu mpango huo unapuuzilia mbali uwepo wao.
Ronaldo akataa mshahara wa £1.6m kwa wiki kutoka klabu ya China
Klabu ya Real Madrid ilipewa takriban pauni milioni 250 na klabu ya China ambayo haikutajwa jina ili kumnunua nyota wake Cristiano Ronaldo kulingana na ajenti wake Jorge Mendes.
Amesema kuwa nahodha huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 31 hana haja na mpango huo ambao ulishirikisha mshahara wa kila mwaka wa pauni milioni 85.
Ronaldo alisema kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine 10 mnamo mwezi Novemba baada ya kuandikisha mkataba mpya na Real Madrid hadi Juni 2021.
''Soko la China ni soko jipya.wanaweza kuwanunua wachezaji wengi, lakini haiwezekani kumnunua Ronaldo'', alisema Mendes.
''Cristiano ndio mchezaji bora duniani, ni kawaida kupata maombi'', aliongezea raia huyo wa Ureno.
Chini ya ombi hilo analodai Mendes, Ronaldo angepokea kitita cha pauni milioni 1.6 kwa wiki ikiwa ni mara tatu ya zaidi ya kitita cha uhamisho wa pauni milioni 89 zilizogharimu uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United.
Mendes aliambia Sky Italia: Klabu ya China imetoa pauni milioni 257 kwa Real Madrid na zaidi ya Yuro milioni 100 kila mwaka kwa Ronaldo.
''Lakini fedha sio kila kitu.Klabu hiyo ya Uhispania ndio maisha yake''.
Hatua hiyo inajiri baada ya klabu ya Shanghai Shenhua kutoka China kuthibitisha kwamba imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kutoka klabu ya Boca Juniors.
Shanghai inayofunzwa na aliyekuwa mkufunzi wa Brighton Gus Poyet ,wameripotiwa kukubali uhamisho wa pauni milioni 40 mbali na mshahara wa zaidi ya pauni milioni 310,000 kwa wiki
Rc Ndikilo ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo kuondoka haraka
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na
wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba
serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro
iyo.
Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya mapigani baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi , sasa yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafigaji.
kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,”Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi , Mbunge wa Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha Taratibu hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto Ruvu kuwanywesha maji. Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi kupoteza mazao yao ; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..
Rc Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo hili la kitonga na mkoa wa pwani , mkuu wa mkoa alisema. Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe,walidai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho. ” hata kama ukweli ndiyo uo , eneo la kufuga mkoa wa Pwani linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo laki 2 na nusu.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Ihefi ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugajo walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona Maji na majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo. Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria hakuna aliyejuu. Alitoa tahadhari kuwa atashughulika na hap wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kibuli.
kwa upande wake mbunge wa chalinze mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoingia kinyemela.
Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya mapigani baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi , sasa yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafigaji.
kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,”Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi , Mbunge wa Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha Taratibu hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto Ruvu kuwanywesha maji. Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi kupoteza mazao yao ; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..
Rc Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo hili la kitonga na mkoa wa pwani , mkuu wa mkoa alisema. Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe,walidai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho. ” hata kama ukweli ndiyo uo , eneo la kufuga mkoa wa Pwani linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo laki 2 na nusu.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Ihefi ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugajo walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona Maji na majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo. Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria hakuna aliyejuu. Alitoa tahadhari kuwa atashughulika na hap wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kibuli.
kwa upande wake mbunge wa chalinze mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoingia kinyemela.
wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza
katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika
kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na
wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
Mwanga akizungumza kwa wananchi katika mkutano wa kutatua migogoro ya
wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika
kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua
migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya
Vigwaza
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani
Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani baada ya mkutano wa
kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata
ya Vigwaza
Tamko la ndg. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto kuhusu Rasilimali na Madeni
Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa
ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria
namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za
Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya
Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku
zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na
sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.
Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo,
kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi
wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa
kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi
fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa
Umma.
Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati
Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa
wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya
Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au
kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la
Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.
Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni
ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi
ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu (
public disclosure of leaders’ assets and liabilities) kuwezesha
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa
mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi
kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.
Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli
kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili
kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi
ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa
anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye
hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili
awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016
Subscribe to:
Posts (Atom)