Waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kiasi cha
watu mia moja wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali, katika
kipindi cha siku tatu zilizopita.
Vyanzo vingine vya habari vinasema watu waliouawa ni 40.
Ofisi ya Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila imepinga taarifa hizo, huku
ikiwalaaumu viongozi wa maandamano hayo kwa kuchochea ghasia hizo za
umwagaji damu.
Upinzani nchini humo wamevilaumu vyombo vya usalama kwa kuwashambulia
kwa risasi watu waliokuwa wakiandamana kwa amani juu ya kuahirishwa kwa
uchaguzi wa Rais nchini humo.
Wanaamini kuwa Rais Kabila anajaribu kung'ang'ania madaraka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake.
No comments:
Post a Comment