Michezo
inayowakutanisha watumishi wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI)
itafanyika Mjini Dodoma kuanzia tarehe 14 – 27 Oktoba, 2016 katika
viwanja vya Jamhuri, Chuo Kikuu Huria, Don Bosco, Chuo kikuu cha
St.Jones, Magereza na Shule za Sekondari za Jamhuri, Central na Dodoma.
Michezo itakayoshindaniwa ni: Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvuta Kamba, Riadha, Baiskeli, Karata, Bao, Drafti na Darts.
Ratiba ya Michezo ya ufunguzi ;
Mpira wa Miguu – Wizara ya Elimu itakutana na Ofisi ya Mkaguzi mkuu wa
Hesabu za Serikali, Netboli- Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa
Umma itacheza na RAS- Manyara, Kuvuta Kamba Wanaume – Ofisi ya Rais –
Ikulu watavutana na Ofisi ya Bunge na Kamba wanawake RAS Iringa
watavutana na Wizara ya Afya.
Kabla ya Michezo hiyo
asubuhi itatanguliwa na Ibada maalum itakayofanyika katika Uwanja wa
Jamhuri ya kumwombea Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere
pia kumtakia afya njema Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wasaidizi wake katika
kuliongoza Taifa letu kwa mafanikio, baada ya tukio hilo Kutakua na
zoezi la kupanda Miti. Nawakaribisha Wakazi wote wa Dodoma kujitokeza
kwa wingi katika viwanja vilivyotajwa hapo juu ili kupata burudani.
Hakutakuwa na kiingilio.
Aidha, naviomba Vilabu kukamilisha taratibu za usajili mapema iwezekanavyo kama ilivyoelekezwa awali.
Moshi Y. Makuka
KAIMU KATIBU MKUU – SHIMIWI.
Imetolewa leo tarehe 28 Septemba, 2016
No comments:
Post a Comment