Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya
matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania
Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi
leo ,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya
upatikanaji wa tiketi za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu
Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho
Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom
Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akieleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi
za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa
Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex
Nkenyenge.
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Mashabiki wa soka nchini
wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa
ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na
kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa
tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
Wasiwasi huo umetolewa na Waziri
wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu
matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania
Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna
kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya
kazi katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi kulalamika kukosa
tiketi za mchezo wa kesho.
“kwa kila anayetaka kwenda
uwanjani kesho kadi zinapatikana nimewaagiza Selcom wahakikishe
wanazungusha magari yao mtaani kuangalia mahali penye upungufu na
yawe na watu wenye kadi hizo aidha, watu waongezwe kwenye vituo ambayo
vina idadi kubwa ya wateja wanaohitaji kadi” Alisema Mhe Nnauye.
Aidha Waziri Nape Nnauye
amewahakikishia watanzania kuwa atausimamia mfumo huu kikamilifu na kwa
gharama yoyote na atahakikisha hautakuwa na mapungufu na endapo
yatajotokeza yatashughulikiwa na wataalamu ili kuufanya mfumo huu
kufanya kazi ipasavyo kama ulivyokusudiwa.
Kwa upande wake Meneja Mradi
kutoka Selcom Tanzania Galius Runyeta amefafanua kuwa mfumo huu uko
wazi kabisa kwa wadau wote wanaohusika na mapato ya uwanjani na utakuwa
njia mbadala ya kudhibiti mapato yatokanayo na mechi.
“ Kwa mfumo huu hakuna njia ya
mkato kila kitu kiko wazi na kwa kila dakika utaona mabadiliko ya idadi
ya tiketi zinazonunuliwa na mpaka sasa zaidi ya tiketi 10,000
zimenunuliwa na zinazidi kununuliwa” Alisema Runyeta.
Kwa miaka mingi kumekuwa na
malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuwepo kwa upotevu wa mapato
katika mechi za ligi na kimataifa katika viwanja vya soka nchini kwa
kuliona hilo Serikali iliamua kuanzisha mfumo utakaomaliza tatizo hilo
na kukomesha mianya yote ya ulaji iliyokuwepo katika mfumo uliopita.
No comments:
Post a Comment