Mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya Equator SUMAJKT kilichopo Ruvu Mkoani Pwani, Robert Mangazeni
akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda kutembelea na kujua
hatua ilipofikia ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha matrekta pamoja na
kutengeneza magari ya zimamoto. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KAMPUNI ya equator
SUMAJKT iliyoko Ruvu, mkoani Pwani, kwa mara ya kwanza itaanza
kuunganisha matrekta ya farmtrac hapa nchini baada ya kuingia mkataba wa
uhawilishaji teknolojia na kampuni inayotengeneza matrekta hayo ya
Escort ya India.
Kupitia makubaliano
hayo equator SUMAJKT itaweza kuunganisha matrekta kwa ajili ya soko la
Tanzania na masoko ya bara la Afrika kwa ujumla.
Akizungumza na
waandishi wa habari, waliokwenda kutembelea kiwanda hicho, mkurugenzi
mtendaji wa kampuni hiyo Robert Mangazeni alisema awali matrekta
yalikuwa yakiletwa kutoka India.
Alisema lakini baada ya
makubaliano hayo kampuni hiyo haitaleta tena matrekta hapa nchini
badala yake yataunganishwa katika kiwanda hicho cha kampuni ya Equator
SMJKT.
” Hatujawahi kuwa na
kiwanda wala karakana za kutengeneza matrekta hapa nchini,
yanapohabirika hutengenezwa kiwango cha chini na mafundi wasio na
ujuzi,”
“Mara nyingi
yakishindikana huegeshwa na kutelekezwa baada ya kushindwa kufanya
Kazi, kwa mara ya kwanza equator SUMAJKT tutafanya Kazi hiyo,
tunayetengeneza pia kuyahudumia yanapoharibika, “alisema Mangazeni.
Alisema matrekta hayo
watayauza wakulima kupitia wakala wao kwa bei nafuu lakini pia
watakopesha wakulima walipe kidogo kulingana na uwezo wa kila mtu ili
kusaidia waweze kulima kilimo chenye tija na kupata kipato na faida.
Aidha Mangazeni alisema kiwanda hicho kinatarajia kuanza kazi rasmi mwezi novemba.
Alielezea kuwa mbali na
kazi yaykuunganisha matrekta pia kiwanda hicho kitaunganisha mabasi, na
magari mbalimbali, pia zana za kilimo.
” Tunatarajia
kushirikiana na viwanda vya ndani kwa ajili ya kuzalisha vipuli
mbalimbali vya magari, matrekta na zana za kilimo, tunategemea
kushirikiana na kampuni ya Automech, kiwandacha TATC- Nyumbu, SIDO,
UDSM na vingine.
Alisema wataalamu
kutoka nje kwa ajili ya ufungaji wa mitambo wameshafika na hatua za
awali za ujenzi wa majengo ya kiwanda hicho na usimikaji wa mitambo na
vifaa zimeshaanza.
Mangazeni alisema hadi
sasa zimeshatumika kiasi cha sh.bil 2,ambapo hadi kukamilika kwake
mwishoni mwa mwezi novemba kinatarijia kutumia bil.3.
Kampuni ya equator
SUMAJKT ni ubia kati ya shirika la uzalishaji mali la JKT (SUMAJKT) na
kampuni ya equator Automech ambayo ni ya watanzania wakiwamo wastaafu
kutoka jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
No comments:
Post a Comment