Ahmed Mahmoud- Arusha
MFUKO wa hifadhi ya jamii NSSF,mkoa wa Arusha,umezifikisha taasisi Nne mahakama ya hakimu mkuu mkazi Arusha,kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa vipindi tofauti zaidi ya shilingi bilioni moja.
Mwanasheria
mwandamizi wa NSSF, Selestini Ntagale, ameiambia mahakama ya hakimu
mkuu mkazi kuwa taasisi hizo zimeshindwa kuwasilisha malimbikizo ya
michango ya wafanyakazi hao kwenye mfuko huo licha ya kukumbushwa mara
kwa mara.
Aliiambia
mahakama hiyo kuwa michango ni haki ya mfanyakazi lakini kampuni hizo
zimekuwa zikiwakata kwenye mishahara na haziwasilishi michango hiyo
hivyo NSSF,kulazimika kutumia sheria kwa kuzifikisha mahakamani ili
mahakama iziamuru kuwasilisha michango hiyo.
Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na ,Water Solution, Net Health, na Hotel ya Snow Crest zote za Arusha.
Ntagale,
aliiambia mahakama hiyo kuwa Kampuni ya Pride Tanzania, tayari ndani ya
siku mbili imeshalipa shilingi milioni 180 kati ya deni lake la milioni
709 .
Ntagale,
alisema Hotel ya Snow Crest inadaiwa tangia mwaka 2015 ambapo
imechelewa kutekeleza hukumu iliyotolewa na hakimu mkazi na hivyo NSSF
kukaza hukumu ambapo kama itashindwa kutekeleza NSSF itaomba kibali cha
mahakama cha kuiuza hotel hiyo kwa njia ya mnada ili kulipwa malimbikizo yanayodaiwa.
Aidha taasisi zingine zikiwemo Water Solution inadaiwa shilingi milioni 83.143.813,Hotel
ya Snow Crest inadaiwa shilingi 449 na Net Health, inadaiwa shilingi
milioni 14, 743,376,madeni ambayo ni malimbikizo yanayotokana na makato ya mishahara ya wafanyakazi ambayo hayajawasilishwa NSSF.
Wakili
mwandamizi, Method Kimomogoro, ambae anaiwakilisha kampuni ya Pride
Tanzania, ameaiambia mahakama kuwa wateja wake wanakubaliana na deni
hilo na watalilipa ndani ya mwezi mmoja .
Kimomogoro, aliiambia mahakama kuwa mteja wake amepewa muda mfupi wa siku mbili na
baada ya kupata taarifa hiyo wamelipa kiasi hicho cha fedha hivyo
anaomba apewe muda wa mwezi mmoja hadi Novemba 4 wawe wamemaliza kiasi
kilichobakia.
Katika hatua nyingine mahakama imetoa hati
ya kukamatwa kwa kampuni ya Net Health, ambayo haikufika mahakamani
hapo huku kampuni ya Water Solution imeyakataa madai hayo ya NSSF
wakidai sio sahihi .
Akiahirisha
kesi hiyo, hakimu mkuu mkazi, Augostino Rwizila, amewataka wadaiwa wate
kulipa madeni yao ndani ya muda wa mwezi mmoja ambapo ameahirisha kesi
hiyo hadi Novemba 4 mwaka huu.
Kwenye kesi hiyo kila mdaiwa ana kesi yake binafsi kulingana na madeni yake ingawa zote zinasikilizwa na hakimu mmoja .
Kesi
hizo ni kama ifuatavyo, Net Health kesi namba, 389/ 2016, Pride
Tanzania limited, kesi namba, 388/ 2016, Water Solution kesi namba, 390/
2016 na Hotel ya Snow Crest kesi namba 61/ 2015 .
No comments:
Post a Comment