Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawsiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akitoa maelekezo kwa Bodi
mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakati alipoitambulisha Bodi
hiyo, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng.
Edwin Ngonyani na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Eng. Leonard Chamriho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi ,
Uchukuzi na Mawasiliano, Eng.Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa
Wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya
kutangazwa kwake leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shrika
la ndege Tanzania (ATCL), Emmanuel Korosso akitoa maelezo kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani)
mara baada ya kutambulishwa kwake leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya
Shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati
wa utambulisho wao leo jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi mitatu kwa Bodi mpya ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kusuka upya uongozi uliopo ili
kuweza kuleta ufanisi wa utendaji kazi wa Shirika hilo.
Akizungumza jijini Dar es salaam
mara baada ya kuitambulisha Bodi hiyo, Waziri Mbarawa amesema kuwa
Uteuzi wa Bodi hiyo utasimamia kuleta tija na ufanisi wa shirika hilo
ambalo kwa kipindi kirefu lilikuwa na changamoto nyingi.
“Nataka kuona mabadiliko makubwa
kuanzia kwenye Menejimenti hadi uongozi wa chini, hakikisheni mnaweka
uongozi amabao utafuata maadili, utakuwa na ufanisi, ubunifu na kasi
katika utendaji kazi” amesema Profesa Mbarawa.
Aidha, ameitaka Bodi hiyo
kusimamia na kuboresha mpango wa kibiashara wa usafirishaji (Business
Plan) katika Shirika hilo ili kuweza kumudu soko la ushindani na kuweza
kuongeza mapato ya Shirika hilo.
“Kama mnavyojua usafiri wa anga
una ushindani mkubwa, hivyo ili Serikali iweze kupata faida katika
biashara hii ni lazima tuboreshe mpango wa kibiashara unaoendana na
wakati”, amesisistiza Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa ameitaka Bodi
hiyo kuipa ATCL mifumo imara, makini na mahiri ili kuweza kutatua
changamoto zinazoikabili Shirika hilo ikwemo wizi wa mafuta ya ndege na
upotevu wa mapato.
Ili kupima ufanisi wa utendaji wa
Shirika hilo Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuandaa mkataba kwa
kila mfanyakazi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
Katika hatua nyingine Waziri
Mbarawa amesema kuwa Serikali ina mpango wa kununua ndege mbili mpya
aina ya Jet ifikapo mwaka 2017 kwa lengo la kuboresha sekta ya
usafirishaji wa anga nchini.
Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ameitaka Bodi hiyo
kutumia fursa walioipata katika kufanya kazi vizuri ili kufufua shirika
hilo na kuwapatia watanzania huduma sahihi na bora za usafirishaji.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo
Mhandisi Emmanuel Korosso, ameahidi kushirikiana na wajumbe wa bodi yake
katika kutekeleza maelekezo ya Waziri haraka iwezekanavyo ikiwemo
kubadilisha menejimenti ya shirika hilo
No comments:
Post a Comment