Thursday, 22 September 2016

Wakazi wa Mtwara wajitokeza kujisajili kupata vitambulisho vya utaifa

msk1
Wawakilishi wa Taasisi, Mashirika na Wizara za Serikali zenye ofisi mkoani Mtwara wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara  (hayupo pichani) wakati akizindua zoezi la usajili Watumishi wa Umma mkoani humo
msk2
Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mtwara wakishiriki sherehe za uzinduzi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma mkoani Mtwara
msk3
Mmoja  wa washiriki akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa watumishi wa Umma mkoani Mtwara
msk4
Washikiri wa sherehe za uzinduzi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma, mkoa wa Mtwara wakilisikiliza kwa makini maelezo ya namna ya kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa
msk5
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akifafanua jambo wakati  wa uzinduzi zoezi la Usajili Watumishi wa Umma mkoa wa Mtwara; lililozinduliwa rasmi Mkuu wa Mkoa huo Bi. Halima Dendogo
msk6
 Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akizungumza jambo wakati wa kuzindua zoezi la usajili wa Watumishi wa Umma mkoani Mtwara
msk7
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Khatib Malimi Kazungu akisikiliza kwa makini majadiliano wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili watumishi wa Umma  mkoa wa Mtwara
msk8
Meneja Usambazaji Vitambulisho vya Taifa Bw. George Mwandezi akitolea ufafanuzi jambo kuhusu usajili  Watumishi wa Umma utakaoanza Octoba 03/2016 mkoani Mtwara

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Mtwara, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujisajili, kama wakazi hawa wa Wilaya za Tandahimba na Newala walivyokutwa  wakishiriki kikamilifu kujisajili.
Moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza ni wakazi wengi hususani maeneo ya vijijini kukosa mashine za photocopy, huku baadhi wakikosa nyaraka muhimu za kuwatambulisha. Changamoto nyingine ni waombaji wengi kutokuwa na taarifa sahihi za umri wao binafsi na wazazi huku baadhi wakikosa taarifa sahihi za maeneo wanakoishi.
Hata hivyo kwa maelekezo na mafunzo yaliyotolewa na NIDA kwa maafisa wote wanaoendesha zoezi hilo changamoto nyingi zimeweza kutatuliwa kutokana na miongozo na madodoso yanayomsaidia mwombaji kutambua baadhi ya taarifa muhimu. Hata hivyo NIDA imewaomba wananchi katika maeneo mengine ambayo zoezi hili halijafanyika kuanza kujiandaa kwa kuwa na nyaraka muhimu zinazoweza kuwatambulisha mathalani; cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti, Kadi ya Bima ya Afya, nambari ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kuwa taarifa sahihi zinazomhusu mwombaji binafsi na wazazi, majina, tarehe na miaka ya kuzaliwa. Picha na Rose Mdami  ( NIDA)

No comments:

Post a Comment