Kwenye kipengele cha Afrika, Tanzania imeorodheshwa kwenye vipengele 17 kati ya 32. Washindi wa tuzo hizo watapataikana kutokana na kura zitakazopigwa kw anjia ya mtandao kwa kuwashirikisha wataalamu wa masuala ya utalii pamoja na wateja.
Msemaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Geofrey Tengeneza alisema: ”Pazia limefunguliwa tangu Septemba 23 na litafungwa Oktoba 24. Kila Mtanzania anaweza kupiga kura kwa kuitembelea tovuti ya WTA na kupiga kura kwenye vipengele vya dunia na Afrika ili kuuleta ushindi nyumbani.”
Miongoni mwa vipengele ambavyo Tanzania imeorodheshwa ni nchi bora ya kuitembelea, ufukwe na kisiwa bora zaidi (Zanzibar), hoteli ya kifahari na kampuni ya utunzaji wa mazingira.
Tuzo hizi zinatolewa miezi mitano baada ya Mlima Kilimanjaro kuchaguliwa kivutio bora zaidi kwa Afrika na nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi zilizofanyika Zanzibar, Aprili 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment