Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri, uzembe na utovu wa nidhamu.
Mwambe
amefanya uamuzi huo alipokuwa kwenye Mkutano na Wafanyakazi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo Tarehe 29.09.2016, ambapo aliwataja
Watumishi hao aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkuu wa Idara ya Ugavi Bw.
Genesius Rugemalira ambaye amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia
manunuzi ya Halmashauri na kuisababishia Serikali hasara ya Tshs. Mil
16, Daktari John Amita wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni aliyesimamishwa
kazi kwa tuhuma za kupigana na daktari mwenzake hospitalini hapo,
tuhuma za utoaji mimba, na uzembe uliopelekea kifo cha mama mjamzito.
Wengine
waliosimamishwa ni Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni Bw. Mika
Iloti kwa uzembe uliopelekea kifo cha Mama mjamzimzito, Msaidizi wa
Ofisi Bw. Anthony Sanga kwa ufujaji wa mapato ya Halmashauri na Mtendaji
wa Kijiji cha Makasuku Bw. Mussa Ndahani ambaye kwa kushirikiana na
Mwenyekiti wa Kijiji chake wamekuwa wakitoa vibali vya uvunaji Misitu
kwa Wafanyabiashara ya mbao bila kuzingatia sheria na taratibu kwa kofia
ya zoezi la utengenezaji wa madawati linaloendelea.
Mh.
Mwambe amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
kuhakikisha Watumishi hao wanasimamishwa mara moja kupisha uchunguzi wa
tuhuma zinazowakabili ili hatua Zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni ametoa karipio kali na kumwagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bw. Charles
Edward Fussi kuwachukulia hatua Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt.
Francis Mwanisi kwa kuficha taarifa na kufumbia macho matukio ya utovu
wa nidhamu wa Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni na
Mhasibu Mkuu wa mapato Bw. Elias Mwachinyemba kwa kushirikiana na
wazabuni wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri waliomaliza muda wao
kuhujumu mapato ya Halmashauri.
Mh.Mwambe
pia ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Manyoni, Bw.
Yona Chalinze na Kaimu Mhandisi wa Maji Bw. Musoma Kanyere kwa utendaji
kazi usioridhisha.
Akitoa
maamuzi hayo Mh. Mwambe amewaeleza Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Manyoni kuwa ni lazima waelewe kuwa wao sio tu Watumishi wa Serikali
bali ni Watumishi wa Umma hivyo wana wajibu kuutumikia umma kwa weledi,
kujituma, uadilifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea lakini pia kuepuka
vitendo vya Rushwa.
No comments:
Post a Comment