Friday, 30 September 2016

Wastara apata shavu la ubalozi wa kampuni mpya ya simu

Wastara akionyesha mkataba
Malkia wa filamu Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampuni ya simu za mkononi ya KZG Tanzania yenye makao makuu yake nchini China.
Katika mkataba huo mwigizaji huyo atavuna kiasi cha tsh milioni 400 kwa miaka miwili akiwa balozi wa kampuni hiyo kwa matangazo na matamasha mbalimbali.
Akiongea na Filamu Central meneja mauzo wa kampuni ya KZG Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa kamapuni yao imelenga kusambaza teknolojia vyuoni kwani wana bidhaa nyingi ambazo zinatumika katika kufundishia wanafunzi hao.

“Leo pia tunazindua simu ya kipekee kabisa kufika hapa nchini Kzg Kimi ambayo inatumia betri ya ndani kwa ndani ambayo ina sifa ya kutengenezeka tofauti na zingine ambazo betri zake zikiharibika hazitengenezeki,”alisema Kalikawe.

Pia Wastara ameishukru kampuni hiyo kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zilizalishwazo na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Computer na vifaa vingine vya teknolojia.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na wasanii wa Bongo movie wakimpongeza Wastara kuingia mkataba huo.

No comments:

Post a Comment